Kiungo wa Chelsea, Conor Gallagher amewaambia mabosi wa timu hiyo kwamba hawatamlazimisha kuondoka katika dirisha hili kwani bado anaamini ana nafasi ya kupambana katika kikosi cha kwanza cha wababe hao wa darajani.

Conor ambaye anawindwa na Atletico Madrid, Aston Villa na Tottenham, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2025.

Licha ya Chelsea kutaka kumuuza Conor ni mmoja kati ya wachezaji walioonyesha kiwango bora katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kwa msimu uliopita.

Matajiri hawa wa Jiji la London wanataka kumuuza kwa ajili ya kujipatia pesa ambazo zitawaweka katika hali nzuri ya kiuchumi kutokana na kesi zinazowakabili.

Msimu uliopita staa huyu wa kimataifa wa England amecheza mechi 51 za michuano yote, amefunga mabao saba na kutoa asisti tisa.

Gallagher alionyesha kiwango bora kabisa msimu wa 2021–2022 wakati akiitumikia kwa mkopo klabu ya Crystal Palace akitokea Chelsea ambayo alijiunga nayo tangu akiwa kinda mwaka 2008.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement