Chelsea imeendelea kufanya mazungumzo na kipa wa Everton, Jordan Pickford, 30, ili kumshawishi ajiunge nao dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa ajili ya kuboresha eneo lao la beki.

Pickford ni mmoja kati ya makipa walioonyesha kiwango bora msimu huu na hadi sasa anashika nafasi ya pili kwa kucheza mechi nyingi bila ya kuruhusu bao akiwa amefanya hivyo katika mechi 12 za EPL, nyuma ya David Raya.

Kipa huyu amekuwa tegemeo kikosi cha timu ya taifa ya England na timu yake na msimu huu amecheza mechi 40 za michuano yote.

Licha ya uwepo wa Djordje Petrovic na Robert Sanchez, benchi la ufundi la Chelsea limeonyesha kutoridhishwa na viwango vyao, hivyo wanahitaji kufanya maboresho zaidi.

Mkataba wa Pickford unamalizika mwaka 2027 na Everton huenda ikahitaji zaidi ya Pauni 50 milioni kwa ajili ya kumuuza.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement