Klabu ya Biashara United imemtambulisha mchezaji wao mpya Ramadhan Mzee Kiparamoto.

Ramadhan Mzee Kiparamoto mtaalamu kwa NBC Championship League amejiunga na Biashara United akitokea katika klabu ya Pan Africans Fc

Ramadhan Mzee Kiparamoto aliwahi kuhudumu katika klabu kadhaa za ligi ya NBC Championship ikiwemo Green Warriors Fc, Pan Africans Fc na sasa ni rasmi yupo Biashara United Fc.

Ramadhan Mzee Kiparamoto ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa ili kuongeza nguvu katika klabu ya Biashara United.

Hapo hapo Klabu ya Biashara United imefanikiwa kunasa saini ya Mchezaji Mpapi Nasib Safari ya Soka ya Mpapi Nasib ilianzaia Baruti Fc ya Musoma na baadaye akajiunga na klabu ya Biashara United na alifanikiwa kuipandisha timu ligi kuu.

Baada ya hapo alijiunga na klabu ya Kagera Sugar na sasa timu ya Biashara United imemrudisha tena kijana kwenye viunga vya Kumbukumbu ya Karume ambayo ni Maskani ya Wanajeshi wa Mpakani Biashara United.

Mashabiki wa Biashara United wamekua na neno moja kwa mchezaji Mpapi Nasib baada ta kurudi na kuichezea tena Biashara United kuwa Mtoto amerudi nyumbani.

Mchezaji Karim Bakiri Mfaume 'Chonto Master' ametambulishwa rasmi na klabu ya Biashara United

Karim Mfaume ni kijana mwenye uzoefu wa soka la Ushindani na aliwahi kuhudumu katika klabu ya katika Alliance ya Mwanza, JKT Tanzania pamoja na Kagera Sugar na timu hizi zote zikiwa ligi kuu ya Tanzania Bara

Msimu huu alianza kucheza soka katika klabu ya Mbuni Fc ya Arusha na alionyesha uwezo mkubwa sana na kuvutia timu nyingi sana lakini klabu ya Biashara United ilifanikiwa kunasa saini yake

Sasa ni rasmi Karim Bakiri Mfaume ni Mwanajeshi Mpya wa Mpakani.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement