BEKI kisiki wa Lille Leny Yoro, 18, ameendelea kushikilia msimamo wake wa kutaka kujiunga na Real Madrid kama ndio kipaumbele chake licha ya uwepo wa vigogo wengine wanaohitaji huduma yake.

Yoro ni mmoja kati ya mabeki walioonyesha kiwango bora katika kikosi cha Lille na Ligi Kuu Ufaransa kwa msimu uliopita.

Mbali ya Madrid ambayo anatamani sana kujiunga nayo saini yake pia inawindwa na Liverpool na Manchester United.

Yoro amewaambia watu wake wa karibu kwamba anahitaji kujiunga na Madrid kwa sababu ndoto yake ni kuchukua mataji makubwa ambapo haoni kama itatimia kama akitua kwenye hizo timu nyingine zinazomhitaji.

Hadi sasa bado kuna mazungumzo yanaendelea baina ya wawakilishi wa beki huyu na mabosi wa Madrid juu ya uwezekano wa dili hili kukamilika.

Mkataba wa Yoro mwenye umri wa miaka 18, unatarajiwa kumalizika mwaka 2025.

Msimu uliomalizika alicheza mechi 44 za michuano yote na kufunga mabao matatu.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement