Mkataba mpya wa staa huyo ambaye jina lake halisi ni Ibrahim Hamad Bacca, unakoma mwaka 2027.

Amewaambia mashabiki kwamba wajiandae kuona ubora zaidi kutoka kwake kuanzia kesho dhidi ya Al Ahly kwani kwasasa ana mzuka wa aina yake.Bacca alijiunga na Yanga dirisha dogo la usajili msimu wa 2021/22 akitokea KMKM ya Zanzibar, baada ya kuonyesha kiwango kizuri kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi 2022 na juzi klabu ilimuongezea mkataba wa miwili huku mechi ijayo dhidi ya Al Ahly imepewa jina lake ili kuhamasisha mashabiki.

Alisema kucheza pamoja na manahodha wake Dickson Job na Bakari Mwamnyeto amekuwa akijifunza mengi na kuongeza na ujuzi alionao hiyo ndio siri ya kuaminiwana kupewa mkataba mpya.

Bacca amesema sio rahisi kuaminiwa na Yanga, lakini yeye kapata hiyo nafasi tena kwa muda mrefu ameahidi kupambana kuhakikisha anakuwa mmoja wa wachezaji watakaokumbukwa kwenye historia ya klabu kama wachache waliomtangulia. "Kuongezwa mkataba wa muda mrefu ndani ya klabu kubwa ambayo ina ushindani mkubwa kwenye eneo ninalocheza kutokana na kuwa na wachezaji wazuri kunanipa nguvu ya kupambana na kuwapa kile wanachotarajia kutoka kwangu" alisema Bacca na kuongeza;

"Ubora waliouona na kuniamini kwao naahidi sita waangusha nitapambana kuhakikisha napata nafasi ya kuutumikia mkataba wangu kwa kuvuja jasho uwanjani na kuipa timu matokeo." Bacca alisema ubora wake unatokana na ushirikiano mzuri na wachezaji wenzake na amekuwa mwepesi wa kujifunza kuliko kuyjiona amekua kutokana na kupata nafasi hivyo anawashukuru wachezaji wenzake kwa kumpa muongozo. Nimewakuta wamekuwa viongozi wangu kwenye uchezaji nashukuru wote nimepata nafasi ya kucheza nao wanamchango mkubwa kwenye ukuaji wa kipaji changu nitaendelea kujifunza na kuwa miongoni mwa wachezaji watakaoipeleka timu pale wanapotamani kufika; “Nina deni kubwa kwa wanayanga kwa mkataba huu mpya sitawaangusha nitaendeleza pale nilipo na kuwa bora zaidi lengo ni kuona nautumikia mkataba kikamilifu kwa kuvuja jasho." alisema Bacca.

Alisema wanakumbushana majukumu bila kujali ukubwa na uzoefu ndio kitu kinachowafanya wawe bora eneo la nyuma ya timu hiyo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement