KLABU ya Azam imekamilisha usajili wakiungo, Adolf Bitegeko aliyekuwaanaichezea timu ya Volsungur IF ya nchini Iceland.

Nyota huyo aliyewahi kukichezea kikosihicho akiwa akademi amerejea nchinibaada ya mkataba wake kumalizikahuku akiwa ni miongoni mwa majinayaliyoitwa na Kocha wa Stars, Adel Amrouche kwa ajili ya AFCON inayoendelea Ivory Coast ingawahakupenya.

Usajili huo ni wa kwanza kwa wachezajiwazawa katika dirisha dogo la usajililililofungwa Januari 15 huku akiwa niwa nne baada ya, Mohamed Mustafa kutoka Al-Merrikh, Yeison Fuentes(Leones FC) na mshambuliaji, Franklin Navarro kutokea Cortulua FC.

Mbali na kuichezea Volsungur IF, timu nyingine alizochezea kiungo huyo ni KR Reykjavik na Keflavík IF zote za Iceland.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement