Uongozi wa Azam FC umethibitisha kupokea ofa kutoka katika timu za Simba SC ya Tanzania na Al Hilal ya Sudan, zikihitaji huduma ya straika wake Prince Dube.

Katika taarifa iliyotolewa leo, Azam FC imesema inazifanyia kazi ofa hizo huku ikiweka milango wazi kwa timu nyingine zitakazomuhitaji mchezaji huyo raia wa Zimbabwe.

Dube ambaye bado ana mkataba na Azam FC wa miaka miwili na nusu, aliandika barua ya kuomba kuondoka klabuni hapo, na uongozi wa Azam FC ulimjibu mchezaji huyo na kumpa masharti ambayo yalikuwa ni kulipa Dola 300000 ambazo ni fedha za kuvunja mkataba huo na kama akishindwa basi aendelee kuitumikia Azam hadi pale mkataba utakapoisha.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement