Mshambuliaji kinda wa klabu ya Yanga ameripotiwa kutakiwa na Klabu ya Azam fc huku Wanalambalamba hao wakidaikwa kupeleka ofa ya milioni 400 (400m) kama ada ya usajili kwa Mzize kwa lengo na kumng'oa jangwani.


Hatua hiyo imepelekea klabu ya Yanga kwenda mezani na nyota huyo kwa ajili ya mazungumzo ya nyongeza ya mkataba mpya wa kuendelea kumbakisha Jangwani.

Ikumbukwe kuna za chini chini kuwa klabu ya Watford ya England nayo ilimfuata Meneja wa mchezaji huyo, Jasmine Razack wakihitaji huduma ya kinda huyo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement