Arsenal imeripotiwa kufanyia kazi kipengele cha kumsajili jumla kipa wa Brentford na timu ya taifa ya Hispania anayeiwakilisha nchi yake kwenye Euro huko Ujerumani, David Raya baada ya kuvutiwa na kiwango alichoonyesha alipokuwa akiichezea kwa mkopo msimu uliopita.


Brentford ilikuwa inataka kumrudisha lakini Raya mwenyewe hakuwa tayari kurudi katika kikosi hicho.

Raya alikuwa ndio kipa tegemeo akichukua bafasi ya Aaron Rasmdale ambaye alitumika kama kipa namba mbili pale Emirates.

Inaelezwa Arsenal inataka kutoa zaidi ya Pauni 20 milioni kwa ajili ya kumsainisha kipa huyu mkataba wa kudumu.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amevutiwa sana na staili ya uchezaji wa Raya ambaye huwa na uwezo mzuri wa kucheza na mpira mguuni.

Mkataba wa sasa wa Raya na Brenford unatarajiwa kumalizika mwaka 2025.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement