AMORIN AHITAJI KUBAKI MAN U ITED KWA MIAKA 20
Akizungumza kuelekea msimu mpya unaokuja kocha huyo raia wa Ureno amesema anatambua kuhusu mwenendo mbaya wa klabu hiyo kwa msimu uliopita huku akidai kuwa sifa zote zilizomleta klabuni hapo zimefutika na sasa yupo tayari kuanza upya.
Ndio nataka kubaki, nataka kusalia hapa kwa miaka 20 na hilo ndio lengo langu na kwa hakika ninaamini katika hilo. Kuna jambo litatokea na kuna nyakati nitakuwa na Bahati, nimekuwa na bahati sana kwenye kazi yangu kama kocha na wazo langu ni kubaki kwa miaka mingi.”— amesema Amorim.



