Aisha Masaka ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza mwanamke kutoka Tanzania kusajiliwa na timu ya ligi kuu ya wanawake ya England.

Aisha amesaini kandarasi na klabu ya Brighton akitokea BK Hacken ya kutoka Sweden aliyojiunga nayo mnamo mwaka 2022 akitokea kwenye klabu ya Yanga Princess inayoshiriki ligi kuu ya wanawake nchini Tanzania

Mwaka mmoja uliopita Aisha aliweka rekodi ya aina yake kuwa mchezaji wa kwanza mwanamke kutoka Tanzania kucheza michuano ya klabu bigwa ulaya kwa wanawake wakati timu yake ya BK Hacken iliposhiriki michuano hiyo.

Masaka licha ya kuwa mchezaji wa kwanza mwanamke kusaiji mkataba kwenye klabu hiyo anaungana na nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta ambaye aliwahi kupita kwenye klabu ya Aston Villa mnamo mwaka 2019.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement