AC Milan na Juventus zinaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Fiorentina na Morocco Sofyan Amrabat ambaye kwa sasa anaichezea Manchester United kwa mkopo.

Inaelezwa kwamba Manchester United haijaonyesha nia ya kubaki na mchezaji huyo na kumsainisha mkataba wa kudumu aliyejiunga katika dirisha la majira ya baridi, mwaka huu.

Amrabat alijiunga na Man United kwa mkopo uliokuwa na ada ya Euro 9 milioni na kuna kipengele cha kumnunua moja kwa moja kwa Euro 25 milioni.

Juventus ndio imeripotiwa kuwa ya kwanza kutaka kumsajili supastaa huyo, lakini AC Milan imeibuka katika siku za hivi karibuni na ndio inaonekana kuwekeza nguvu kubwa zaidi.

AC Milan inadaiwa kwamba inataka kumsajili Amrabat kwa sababu msimu uliopita ilipitia changamoto kwenye eneo la kiungo hususan katika upande wa kuzuia.

Amrabat alitua Manchester United baada ya Mashetani Wekundu kushinda vita dhidi ya Barcelona ambayo pia ilikuwa inamtaka, na pia imekuwa ikitajwa kutaka kurejea tena ili kumsajili mchezaji huyo baada ya kuona dalili zake za kubaki Old Trafford zinazidi kupungua.

Tangu alipotua katika Man United amekuwa akiingia kutokea benchi, nafasi yake ikikamatiwa kwa sasa na Kobbie Mainoo. Mkataba wake Fiorentina unamalizika 2025.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement