YANGA SC VINARA WA KUBEBA KOMBE LA FA TANGU LIKIITWA KOMBE FAT
UNAWEZA kusema kwamba Klabu ya Yanga ni Baba lao kwenye michuano hii ya Shirikisho, ambapo imechukua ubingwa mara 7, ikufuatiwa na Simba mara 4.
Je miaka yote hiyo wengine walikuwa wapi ?
Kuanzia mwaka 2003 michuano ya FA haikuwa ikichezwa, hadi pale Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania TFF, walipopata udhamini na wa Azam Media na ndipo mwaka 2015 ilipoanza kuchezwa tena, huku Yanga wakiendeleza ubabe wao tangu waanze kulichukua mwaka 1967 lilikuwa linaitwa kombe la FAT ambapo Yanga iliifunga Liverpool ya ILALA Mabao 2-0
Yanga ilitwaa taji la Kwanza la ASFC, kwa ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Azam FC, kabla ya Simba kufanya makubwa kwa kuifunga Mbao FC kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
MIKOA ILIYOWAHIKUCHEZWA FAINALI YA FA
2015-16- Benjamin Mkapa, Dar Es Salaam.
2016-17-Jamhuri, Dodoma
2017-18- Sheikh Amri Abeid, Ausha
2018-19-Ilulu Lindi.
2019-20-Nelson Mandela, Rukwa
2020-21- Lake Tanganyika, Kigoma
2021-22-Sheikh Amri Abeid- Arusha
2022-23-Mkwakwani Tanga
2023-24- New Aman, Zanzibar
MABINGWA WA KOMBE LA SHIRIKISHO TANGU LIANZISHWE FAT HADI LEO FA.
๐Yanga SC kachukua mara 8 kuanzia mwaka,
๐1967
๐1974
๐1999
๐2001
๐2015/16
๐2021/22
๐2022/23
๐2023/2024
๐Simba kachukua ubingwa wa FA mara 4 katika historia
๐1995,
๐2016/17
๐2019/20
๐2020/21
๐Azam FC wao wamechukua ubingwa huo mara moja tu mwaka 2018/18.
๐Timu zingine zilizowahi kuchukua ubingwa wa FA,
๐Majimaji 1985
๐Sigara FC, 1996
๐Tanzania Stars 1997, 1998
๐Mtibwa Sugar 2000
๐JKT Ruvu 2002/2003
๐คฃHaikuchezwa, 2017/18
RASMI: YOUNG AFRICANS NI MABINGWA MARA 8 WA KOMBE LA FA TANGU LIKIITWA KOMBE FAT.