Wakati enzi zake akiwa golini alikua imara sana,wengi wetu tuliomshuhudia Kaseja kuna vitu hatukua na uelewa navyo.

Mimi ni mmoja wa watu niliomshudia Kaseja kuanzia ile Simba Sc ya kocha raia wa Kenya James Aggrey Sian'ga.

Kiufupi Kaseja alikua nyanda aliyekamilika sana ukiondoa kigezo cha urefu.

Kipindi hicho hatujui footwork nini faida yake,lakini Kaseja alikua mzuri kwenye matumuzi ya miguu yake kutengeneza mpango kazi kuanzia Low block kwa umaridadi wa juu sana.

Alikua bora sana kuanzisha BUILD UP, pasi fupi fupi kwake uwanja wa nyumbani.. enzi ziile mpira unaoneshwa Star Tv au TVT sasa TBC Taifa mambo yale hatukuyaona kama muhimu.


Nyakati zikasogea, Kaseja akatoka Simba Sc na kujiunga na mahasimu wake Yanga Sc, akaendeleza utamaduni wake ule ule wa kutobutua mali akiwa na mpira mguuni hata akifanyiwa pressing.

Kwenye mechi moja ya mashindano ya NANI MTANI JEMBE,Kaseja alichoma akiwa Yanga kutokea Simba Sc, kujiamini kwake akapiga pasi mkaa,muda sio mrefu akaokota mpira nyavuni mfungaji akiwa Awadhi Juma'Mqniche' sasa kocha msaidizi wa Mtibwa Sugar.

Kuanzia pale maisha yake ndani ya Yanga yalikua magumu na kuonekana kama ameihujumu Yanga Kwenye mechi ile.

Andiko langu limejikita kwa Kaseja kama kipa wa kisasa aliyecheza kwenye nyakati ambazo hatukua na uelewa juu ya matumuzi ya miguu sahihi ya makipa.

Ila baada ya kukumbuka alichokifanya na sasa naona kina Djigui Diarra, Mohamed Mustapha, Aishi Manula, Ngeleka, Wilbol Maseke na wengine wengi ndio nikakumbuka miguu ya Juma Kaseja iliyokua ikipiga pasi kwa usahihi mkubwa.

Always copa haipotei kama asemavyo Juma Kaseja.

Simply Juma Kaseja alikua kipa bora wakati ambao sayansi ya mpira haikua kwa upana na uelewa mkubwa kwa wafuatiliaji.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement