Pengine ushindi huo kwa Yanga usingekuwa rahisi kupatikana kama sio mabadiliko ya kocha wao Miguel Gamondi aliyoyafanya dakika ya 65 wakati timu yake ikiwa nyuma kwa mabao 2-1. Yanga ikiwa nyuma ikitoka kuruhusu bao la penalti iliyofungwa na mshambuliaji Prince Dube,

Azam waliona kama mechi wameimaliza hata kiungo wao Feisal Salum 'Fei Toto akafanya hata ishara kwamba wameshamaliza kazi kwenye benchi la Yanga.

Gamondi alimtoa Mudathir Yahya na nafasi yake akamuingiza winga Jesus Moloko mabadiliko ambayo yalikuwa yanamtoa kiungo mkabaji na kumuingiza kiungo mshambuliaji wa pembeni ili kuongeza kasi ya mashambulizi.

Yanga haikuwa na uhitaji sana wa kukaba wakati huo ikiwa nyuma, Gamondi akiamua kubaki na kiungo mmoja mkabaji Khalid Aucho huku akiongeza idadi wa viungo washambuliaji watakaoharakisha mashambulizi kwenye eneo lao la mbele.

Mpango huo ulilipa kwa Yanga wakasawazisha bao hilo dakika nne baada ya mabadiliko hayo kwa kutengeneza shambulizi zuri lililozalisha pigo la adhabu ndogo nje ya eneo la hatari na staa wao Stephanie Aziz KI akaweka mpira kambani.

Yanga ilitumia dakika 9 tangu mabadiliko hayo kupata mabao hayo mawili ambapo Aziz KI tena akafunga bao la tatu na la ushindi dakika ya 71 wakiwa wameendelea kuipelekea presha kubwa Azam.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement