Ni utafiti mdogo usiohitaji uwekezaji mkubwa wa akili/fikra kutambua kiundani mahusiano mazuri Kati ya umri mdogo na utendaji kazi kwa kiwango cha juu.

Kwenye mpira wa miguu hiki ni kitu muhimu sana na huwa hakijifichi juu ya mchezaji wa rika fulani.


Asilimia kubwa ya wachezaji wa Afrika Magharibi wanakulia kwenye malezi mazuri ya soka tangu wakiwa wadogo hii inachagizwa na utajiri mkubwa wa Football Academies zilizopo kwenye mataifa hayo.

Ndio maana ni rahisi kuona mchezaji wa miaka 18 kutoka mataifa ya Ivory Coast, Nigeria, Cameroon,Ghana,Mali kuwa kwenye timu kubwa nje ya Bara la Africa au kuitwa timu zao za Taifa kutokana na msingi mzuri wa malezi ya kisoka.

Jean Charles Ahoua kijana wa miaka 22 amekuja Tanzania kutafuta changamoto mpya,katika umri wake tayari yupo timamu kupambana na kuweza kushinda.

Huyu amepita kwenye stage zote za upishi wa kuwa mchezaji mzuri au bora 

Kwasasa yupo kwenye stage ya mwisho kuelekea kushinda Baada ya kupita TRAINING TO COMPLETE 

Maana yake yupo timamu kwenye fitness,saikolojia na maendeleo mazuri kiufundi,uimara na udhaifu 

Baada ya hapa mchezaji anahesbika kuwa tayari kimapambano kwasababu ndio umri sahihi ( ni miaka 16+) ndio maana unaona wachezaji wengi barani Ulaya wenye umri wa miaka 16-20 wanakua tayari na kupewa nafasi ya kucheza kuanzia klabuni mpaka timu za Taifa.

TRAINING TO WIN 

Baada ya kupambana maana yake unapaswa kushinda na kwenye mpira wa miguu tunaongea kushinda makombe tofauti tofauti kutokana na ushiriki wa timu katika calendar ya mashindano

Maana yake mchezaji anapewa mechi tofauti tofauti za kiushindani na kupambana kushinda.

Jean Charles Ahoua yupo kwenye umri wa kushinda baada ya kupikwa kufanya hivyo.

Kiungo mshambuliaji huyu ana uwezo mzuri wa kufunga magoli na kutengeneza nafasi za kufunga magoli.

Ana sifa kubwa ya kufunga kutokea mbali (shooting from distance) maana yake ana uwezo mkubwa wa shooting ability+ precision ( usahihi wa hayo mashuti).

Ana passing ability ✅, Ball retention ✅, vision ✅ 

Ngoja tuone ligi ikianza ataanza vipi..

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement