Ni jiji la Dar Salaam mida ya usiku nimekaa nawaza kuhusa Maisha yangu jinsi ambavyo yamejaa mateso na huzuni ,wakati nawaza kuhusu Maisha yangu akatokea binti mmoja na kunishika mkono huku akiniuliza kwanini unaonekana huna furaha ? Nikaanza kutabasamu ili nisionyeshe unyonge mbele yake.

Wakati najitahidi kutengeneza furaha katika uso wangu kusudi mtu mwingine asioneunyonge nilionao, Mara yule Binti akaniambia kuwa hayo unayopitia hata mimi nimewahi kupitia ingawa sijui unasumbuliwa na tatizo gani lakini maumivu ya aina hii nimewahi kuwa nayo ila kitu pekee kilichoniondoa katika hali hiyo ni Nafsi ya kutokukata tamaa, Nikitazama kupambana katika kusaka mafanikio nikiwa kama Binti na Mwanamke Mpambanaji.

Bila kupoteza muda nikamuuliza hayo yote umeyaweza vipi? Ndipo akanieleza juu ya mwanamama aliyeamua kuzikimbilia fursa pasipo ujali jinsia, hadithi yake ya upambanaji inavutia kuisikiliza kila uchao.

Ni Suma Stephen Mwaitenda, mwanamke shujaa, mchapaka kazi, ameupiga mwingi kwa mwaka 2023 na hata miaka mingine iliopita.

Amefanya kazi na taasisi mbalimbali lakini pia amewasaidia watu wengi kwenye Maisha yake kwanzia ushauri na mambo mengine mengi,anapenda kuwaona vijana wakifanya kazi nakuwasaidia kuziona fursa mbalimbali kama ambavyo mwenyewe anaeleza .

Mwaitenda anasema siku zote jitahidi sana kutafuta suluhisho la changamoto zako kuliko kuzielezea tu kwa watu kwasababu sio watu wote ambao utawaambia changamoto zako na wakakuelewa ,anasema jitahidi sana kutumia vizuri muda wako ili uweze kufanya mambo yako kwa ubora wa hali ya juu . 

Suma mwaitenda amewashauri vijana wengi kutokukata tamaa na hii ni nguvu iliyopo ndani yake kutokana na na uimara wake.

Aliweza kujiingiza kwenye michezo na kufanya kazi kwenye Klabu kubwa, bora na yenye mafanikio makubwa ya kushinda mataji mbalimbali hapa nchini.

Alijitosa kuwa mjumbe wa Klabu ya Yanga na baadae akawa mwenyekiti wa kamati ya Habari na baadaye aliweza kufanya mambo mengi makubwa ikiwa ni pamoja na kulifanya tamasha la wiki ya mwananchi kuwa kubwa zaidi na kueleza sababu za kwanini ameamua kulifanya tamasha hili kuwa kubwa 

Ukiacha nafasi hii ambayo ameitendea haki kwa kaisi kikubwa lakini pia SUMA MWAITENDA amehudumu kwenye nafasi mbalimbali ndani ya Klabu ya Yanga na amefanya kazi kwa uweledi wa hali ya juu .

Amefanya kazi Yanga kwa uweledi wa hali ya juu na kuondoa kabisa zile kauli zinazosemwa mtaani kwamba wanawake hawawezi kufanya kazi sehemu zenye pressure kubwa lakini kutokana na uimara wake amefanikiwa kulifanya hilo kwa uweledi wa hali ya juu .

Wanawake wanaweza kufanya mambo makubwa wakiaminiwa na kupewa nafasi, tangua ameanza kufanya kazi yanga ameleta utulivu wa hali ya juu kwenye Klabu hiyo kitu ambacho kilisababisha kuleta maendeleo makubwa zaidi na kuwa moja ya viongozi waliofanikisha Klabu hiyo kupata wadhamini wenye tija na mafanikio.

Suma mwaitenda hakuishia hapo aliamua kuchukua form ya kugombea nafasi ya kuwa makamu wa Raisi wa klabu ya Yanga ikiwa lengo lake ni kuifanya yanga kuwa kubwa na tishio barani Afrika bila kusahau kuwa na uwanja wao binafsi .

Alihamasishwa na kujumuishwa na sasa ni mwanamke anayeleta mwanga wa mafanikio kwa wanawake wengi zaidi.

Sisi TV3 TANZANIA tunaheshimu kazi kubwa ambayo ameifanya kwa ubora wa hali ya juu, licha ya changamoto mbalimbali ambazo amekutana nazo lakini amefanikiwa kuzishinda hata kama hajafanikiwa kuwa makamu wa raisi wa yanga lakini ameonyesha njia kwa wanawake wengine.

Uthubutu wa Mwanamke mmoja, hunyanyua wengi zaidi katika kuonyesha njia ya Mafanikio.

Na sisi TV3, Tunamvisha Taji Mwanamama Suma Mwaitenda, Tunasema Ameupiga Mwingi.


IMEANDALIWA NA: FATUMA RASHIDI

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement