2014 - kwenye kombe la Dunia Brazil , Gabriel Jesus alikuwa mtoto wa mtaani akipaka rangi katika jiji la Sao Paulo. Leo ni tajiri kwa sababu ya soka hili hili tunalipigia kelele 🙆

2000 - Cristiano Ronaldo alikuwa akimsaidia mama yake kuuza McDonald's burgers mtaani huko Ureno lakini leo kwa sababu ya soka ni BILIONEA Kwasasa 🤦

2021 - Mzize alikuwa bodaboda Mkoani Iringa baada ya kumaliza O level Mkoani Tanga, kwa sababu ya soka siku ya Jana nae alikuwa miongoni mwa Wachezaji wa yanga sc waliotinga Bungeni kwa heshma baada ya kutwaa Ubingwa na klabu yake ya Young Africans,

Kwa makadilio akiwa bodaboda alikuwa akiingiza Tsh. elfu 15 kwa siku, leo kwa sababu ya soka amepewa asaini mkataba wa Tsh 10 Milioni kwa mwezi - RESPECT FOOTBALL.

UNATAKA NI KWAMBIE MWAKA GANI 🤣.

Hiyo Picha ilipigwa Mwaka......

Hapo Vijana walikuwa wametoka Mazoezini maarufu Uwanja wa Mochwari ambapo ndipo Taasisi ya Moro Kids ilikuwa ikifanyia mazoezini yao..👏

MAISHA YANA SIRI KUBWA SANA: Hao Vijana kwenye Picha ukimuondoa mwenye Jezi ya Arsenal ambaye nae alikuwa kiungo Hatari wa @morokidsacademy ila yeye hakufanikiwa kufikia malengo yake na sasa ni Tabibu akiwa Jijini Mbeya, anafahamika kwa Jina la gaspinho (Gaspar Tweve),

MUNGU AKIPANGA JUA AMEPANGA: Hao vijana wengine waliosalia kwenye Picha.

👉 kibabage - Yanga Sc

👉 kibwana shomari - Yanga Sc

👉 mshery - Yanga Sc

👉 mkele - mtibwa sugar

NIKUCHEKESHE ILA NDIO MAISHA: Hapo hakuna kijana aliyekuwa na nauli ya kurudi kwao kipindi hicho, nauli ya Daladala (Hiace ilikuwa Tshs. 100 (Mia moja),

Walikuwa wanetoka Mazoezini wanarejea makwao kwa Bahati nzuri nikawa nimewaita kwa Interview kipindi hicho ilikuwa ikifahamika Radio Afrika Swahili ikiwa Katika jengo la MAFAO la NSSF Morogoro ikiwa chini ya MR. Davis Mosha kabla ya kubadilishwa na sasa kujulikana kama Dizzim Fm ambayo ipo chini ya Sallam Sk,

Soka ni AJIRA, soka ni AFYA, soka ni njia rahisi zaidi ya kuwa TAJIRI ILA ukiwa na kipaji na watu sahihi wakukusapoti.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement