Kwanza ni kupata ushindi wa aina yoyote

Mbili ni sare ya kuanzia mabao 3-3

Tatu ni kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti baada ya kulazimisha sare ya mabao 2-2 ugenini. Hata hivyo matokeo hayo yote ya aina tatu yanaonekana sio mepesi kupatikana kutokana na rekodi bora ya kufanya vizuri nyumbani ambayo Al Ahly wamekuwa nayo kuanzia katika mashindano ya ndani hadi ya kimataifa.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa tangu ilipofungwa mabao 2-0 nyumbani na Wydad Casablanca ya Morocco, Mei 30

mwaka jana, Al Ahly haijapoteza mechi nane mfululizo za mashindano ya kimataifa nyumbani, wakishinda michezo saba na kutoka sare moja huku wakifunga mabao 20 na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara mbili tu.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement