Simba juzi ilikuwa mgeni wa Al Ahly katika mchezo wa marudiano wa African Football League uliochezwa Cairo, Misri na kuambulia sare iliyoitoa kwenye mashindano baada ya nyumbani kufungana mabao 2-2.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, Salim Abdallah alisema walitolewa kimchezo, lakini wao kama viongozi hawana deni na mastaa wao kutokana na ubora waliouonyesha.

Alisema wachezaji walipambana kwa jasho jingi, lakini bahati haikuwa upande wao walitolewa katika mashindano, hivyo wanajipanga kwa ajlili ya michezo ijayo siku za usoni ili waweze kufanya vizuri.

"Wachezaji wamecheza, wameonyesha ukubwa wao katika michuano mkubwa inayowakutanisha wakubwa hatuna tunachowadai wamepigana sana

ilitakiwa mshindi apatikane ndio matokeo ya mpira," alisema Mwenyekiti huyo alilipongeza benchi la ufundi kwa namna ambavyo linazidi kukiimarisha kikosi hicho na kuendelea kuwa bora kila siku.

Benchi letu la ufundi ni zuri na tunaliamini lina watu bora na sahihi katika kutufikisha kwenye malengo yetu ambayo tumejipanga kuyafikia," alisema. Simba imekuwa na wakati mgumu wa kunusa nusu fainali na kujikuta ikikwama robo fainali mfupa ambao

umewashinda na wanatakiwa kupambana kuuvunja, ikiwa mara tatu wameishia robo fainali michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement