Hii ilikuwa mwaka 2005 katika mechi ya robo fainali ya UEFA kati ya Ac Milan dhidi ya Inter Milan, mechi hiyo ililazimika iahirishwe kwa muda katika dakika ya 73 ya mchezo baada ya kutokea ghasia, fujo na vurugu kubwa sana katika uwanja wa San siro.

Virugu hizo zilitokea baada ya Esteban Cambiasso mchezaji wa Inter Milan kufunga goli na kukataliwa kabla ya dakika 20 mechi kuisha huku Ac milan wakiwa wanaongoza goli 3 - 0.


Baada ya hilo goli kukataliwa, mashabiki wa Inter Milan walianza kurusha moto uwanjani na kusababisha wingu zito sana la moshi uwanjani na vurugu nyingine zikawa zinaendelea kwa muda dakika 15 hadi 20.

Kilichowashangaza wengi katika hizo vurugu wakati ambao mashabiki wanagombana lakini Marco Materrazi wa Inter Milan ambaye ni moja ya mchezaji mtukutu akiwa na kiungo hatari wa Ac Milan Rui Costa walikuwa wameeka pozi huku wakitazama vurugu hizo.


Marco Materrazi na Rui Costa walipigwa picha ambapo picha hiyo ni moja ya picha ambayo imeacha alama kubwa sana katika mchezo wa soka na nchi ya Italia kwa ujumla. 

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement