Baada ya kuiongoza Manchester City kushinda ubingwa wa Ligi Kuu England kwa mara ya nne mfululizo, Pep Guardiola ameshinda jumla ya mataji 17 tangu atue klabuni hapo.

Man City inakuwa timu ya kwanza katika historia ya Ligi kuu England kutwaa ubingwa mara nne mfululizo rekodi ambayo hata kocha wa zamani wa Manchester United, mkali Sir Alex Ferguson hakuwahi kufikia.

Kwa ujumla Pep Guardiola ameshinda Mataji 12 ya Ligi kwenye Ligi tano bora Ulaya wakati Sir Alex Ferguson akiwa na mataji 13 ya Ligi. Pep anahitaji kushinda ubingwa wa Ligi mara moja zaidi kufikia rekodi.

REKODI YA MAKOCHA WENYE MAKOMBE MENGI LIGI KUU ENGLAND

🏴󠁧󠁢󠁳󠁣󠁴󠁿 13 - Alex Ferguson

🇪🇸 6 - Pep Guardiola

🏴󠁧󠁢󠁳󠁣󠁴󠁿 6 - George Ramsay

🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 6 - Bob Paisley 

🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 5 - Tom Watson

🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 5 - Herbert Chapman

🏴󠁧󠁢󠁳󠁣󠁴󠁿 5 - Matt Busby

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement