Yanga Sc kuna wachezaji wengi bora sana,orodha ni ndefu ya hao wachezaji bora lakini endapo nikiulizwa swali la kutaja wachezaji watatu mpaka wanne muhimu basi kuna huyo mwamba kwenye picha lazima awepo.

Kwenye somo la UCHUMI kuna kitu kinaitwa SCALE OF PREFERENCE,unakua na namba ya mambo ya kufanya na yote ni muhimu lakini kuna moja muhimu zaidi na mengine yatafuata accordingly.

Mfano kwenye vitu hivi vitatu hapa chini 

A. Gari limeharibika tairi 

B. Mtoto anaumwa sana

C. Mama mzazi anaomba msaada wa kifedha kijijini.

Kwenye SCALE OF PREFERENCE,vitu hivi vitatu vyote ni muhimu LAKINI kuna nanna umuhimu unakua unapishana uzito 

Kupitia hivyo vitu vitatu kuna cha kwanza muhimu sana kuliko vingine,na mpangilio utakua kama ifuatavyo

A. Mtoto anaumwa sana,maana yake hapa familia itaangalia swala hili kiupana na kumpeleka hospital.

B. Mama mzazi kupewa msaada litakua jambo la pili kwenye umuhimu kwasababu ya mazingira ya mama anayoishi huko kijijini.

C. Gari kuharibika tairi maana yake familia itachukulia kama jambo la tatu muhimu kwasababu gari kuharibika sio kwamba watakua wamekosa option ya kufanya namna kufika eneo/maeneo tofauti tofauti ya kazi zao.

Kwanini mfano huo hapo juu? Kwasababu ndani ya Yanga Sc hao wachezaji bora wapo wengi lakini ubora na ukamilifu wao unatofautiana.

Kwangu mimi ndani ya Yanga Sc wachezaji wanne/ watano muhimu ni kama ifuatavyo kimpangilio.

1. Pacome Zouazoua 

2. Djigui Diarra 

3. Max Nzegeli 

4. Aziz Ki 

5. Khalid Aucho 

NOTE: Pacome Zouazoua na Maxi Nzegeli ni wachezaji ambao ni ngumu sana kupotezwa kwenye mechi zenye intensity na daraja la juu la mpinzani.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement