Miaka miwili iliyopita nilimaliza katika nafasi ya sita, mwaka jana nikamaliza katika nafasi ya nne, sasa ni zamu yangu” hayo yalikuwa ni maneno kutoka kwa Mario Balotelli wa miaka 20 aliyekuwa anashinda tuzo ya golden boy inayotolewa na gazeti la Tuttosport la Italia.

 Alipoulizwa kuhusu mpinzani wake Jack Wilshere aliyemaliza katika nafasi ya pili.

 Baloteli Alitulia kidogo kisha akavaa ule uBaloteli wake na kusema “ Simfahamu Wilshere ni nani, ila wakati mwingine nitakapocheza dhidi ya Arsenal nitamuangalia kwa ukaribu zaidi, nitamuonesha hii tuzo na kumkumbusha kuwa niliitwaa mbele yake.” Inter Millan walimuuza kwenda Man City wakikumbuka fedhea aliyowafanyia siku chache kabla ya Milan derby.


Baloteli alikwenda kwenye mahojiano na kipindi Fulani cha TV nchini Italia akiwa amevalia jezi ya AC Millan huku akijua wazi kuwa yeye ni mchezaji wa Inter Milan. 

Yaani kama leo, mchezaji wa simba au yanga aende katika Interview na jezi ya mtani wake, Licha ya umri na uwezo wake, Inter Millan walihitaji euro million 19 tu kutoka kwa Man City.

Walishachoshwa na vituko vyake

Mourinho akiwa Inter aliwahi kusema “ningeweza kuandika kitabu cha kurasa 200 kuhusu miaka miwili niliyokaa Inter na Balotelli, ila hicho kitabu kitajaa vichekesho.

 "Nakumbuka kipindi Fulani tulienda kucheza dhidi ya Kazan, katika huo mchezo washambuliaji wangu wote walikuwa majeruhi, nilikuwa katika wakati mgumu sababu nilikuwa na Baloteli peke yake.

 Baloteli alipata kadi ya njano kwenye dakika ya 42, nilipoenda chumbani wakati wa mapumziko nilitumia dakika 14 kati ya 15 za mapumziko kuzungumza na Baloteli peke yake.

Nilimwambia, Mario nakuhakikishia sitakubadilisha sababu sina mshambuliaji mwingine, hivo usimguse mtu, cheza mpira tu, mtu akikuudhi usimsemeshe, referee akikosea usimsemeshe, nakuahidi sitakubadilisha.


Ila tuliporudi uwanjani alionyeshwa kadi nyekundu dakika moja tu baada ya mpira kuanza.” Siku moja alipata ajali akielekea mazoezini. Polisi walipofika eneo la tukio waligundua Baloteli amebeba kiasi cha Euro 5000 kwenye gari lake.

Polisi walipomuhoji kwanini anabeba kiasi kikubwa cha hela namna hiyo ilihali anajua ni hatari kwa usalama wake, Baloteli aliwageukia na kuwaambia “ mnauliza kwanini nimebeba hela nyingi namna hii? ni kwasababu mimi ni tajiri, as simple as that, mimi ni tajiri” alafu akaondoka zake. Utukutu ulioje ul.

Siku moja Balotelli alimchezea rafu mbaya Scott Sinclair wakiwa mazoezini.

Kocha wake Roberto Mancini alimuita pembeni na kumtaka aondoke uwanjani. Baloteli aligoma.

Kilichofuata? Hayakuwa maongezi tena bali mchezo wa mieleka, Walipigana kabali wakikaripiana.  Mancini baadae alisema

“nimemuambia ningecheza na wewe miaka kumi iliyopita ningekupiga ngumi kila siku, zipo njia nyingi za kumsaidia mtoto kama Mario, siongei nae mara kwa mara, sababu nikifanya hivo nitahitaji mwanasaikolojia wa kunisaidia, lakini naongea nae kwasababu sitaki apoteze kipaji chake.

Mario asipokuja kuwa moja ya wachezaji bora duniani itakuwa ni kwasababu ya nidhamu yake. Ninavomtazama, naona ana kila kitu cha kuwa mchezaji bora wa dunia.”


Hayo yalikuwa maono ya Roberto Mancini kwa Mario Balotelli, Ila kwa sasa Balotelli yupo Brescia inayoburuza mkia katika Serie A.

Bila shaka Baloteli atamalizia mpira pale Palermo kwenye club yake ya utotoni ya Lummezene inayoshiriki ligi daraja la tatu Italia.

Siku hiyo atageuka nyuma na kukumbuka mabao yake 114 kwa vilabu alivopita na mabao 14 kwa timu yake ya Taifa.

Kisha atatabasamu atakapokumbuka assist yake kwenda Aguero iliyoipa ubingwa Man City mwaka 2012 dhidi ya QPR. atamalizia kwa kukumbuka bao lake la kwanza kwa Man city kwenye ushindi wa 6-1 pale Old Trafford.

 Atakumbuka alivofunua jezi yake ili ajibiwe swali aliloliandika katika fulana yake ya ndani, “WHY ALWAYS ME?” Swali ambalo Super Mario hajajibiwa hadi leo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement