Jose Mourinho amefichua sababu halisi iliyofanya Mohamed Salah na Kevin De Bruyne kuuzwa na Chelsea wakati akiitumikia klabu hiyo, Maswali mengi yamekuwa yakiulizwa kwa miaka mingi ni kwanini The Blues waliruhusu wachezaji wawili mahiri waondoke Stamford Bridge.

Mourinho alifanya kazi na wote wawili, lakini aliona Salah akiondoka kwenda Roma na De Bruyne kwenda Wolfsburg.

Mourinho ameiambia Obi One Podcast: “Kusema kweli, waliondoka kwa sababu walitaka kuondoka. Waliondoka kwa sababu hawakutaka kusubiri.

"Historia inathibitisha kwamba chaguo lao lilikuwa zuri kwa sababu wamekuwa na kazi walizonazo na kufikia kiwango cha juu, lakini wakati mwingine watoto hufanya maamuzi kama hayo kwa sababu hawawezi kusubiri, au hawana uvumilivu na utulivu ili wasubiri wakati ufaao.

"Walikuwa watoto tu ambao hawakuweza kusubiri, na kazi zao zinasema walikuwa sahihi, lakini haikuwa chini yangu. Labda watu wengine watasema niliwauza, lakini siyo kweli.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement