Kombe la Mataifa ya Afrika ni shindano kuu la la soka la kimataifa katika bara la Afrika. Shindano hili husimamiwa na Confederation of African Football (CAF), na lilichezwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1957. Tangu mwaka wa 1968, shindano hili hufanyika baada ya miaka miwili.

Katika mwaka wa 1957 kulikuwa na mataifa matatu yaliyoshiriki katika shindano hili ambayo ni: Misri, Sudan na Ethiopia. Afrika ya Kusini walikuwa washiriki katika shindano hili lakini walizuiwa kutokana na sera za ubaguzi nchini humo. Tangu wakati huo, mchuano huu umeenea, na kusababisha michuano ya kufuzu. Idadi ya walioshiriki katika fainali ya shindano hili ilifika 16 katika mwaka 1998, timu 16 zilikuwa zishiriki katika shindano hili mwaka wa 1996 lakini Nigeria walijitoa na kubakia timu 15), na tangu wakati huo, imebaki kuwa timu 61 ndizo zinashiriki katika shindano hili. Timu hizi hugawanywa katika vikundi ambavyo kila kundi kina timu nne ambapo timu mbili bora katika kila kundi ndizo zinafaulu katika hatua ya ya pili.

Misri ndiyo taifa lililofanikiwa zaidi katika historia kombe hili kwa kuwa na rekodi ya kushinda kombe hili mara sita. Ghana na Cameroon wameweza kunyakuwa ubingwa mara nne. Nyara tatu tofauti zimetunzwa katika historia ya shindano hili. Ghana na Cameroon wameshinda matoleo mawili ya kwanza baada ya kila timu kushinda shindano hili mara tatu mfululizo. Nyara iliyo sasa ilitunzwa mara ya kwanza mwaka wa 2002.

Chimbuko la Kombe la Mataifa ya Afrika lilikuwa mnamo tarehe Juni 1956, wakati uundaji wa Confederation of African Football ulipendekezwa katika mkutano wa tatu wa bunge la FIFA mjini Lisbon. Kulikuwa na mipango ya haraka kwa mashindano ya mataifa ya bara kufanyika, na mwaka wa 1957 mwezi wa Februari shindano la kwanza la Kombe la Mataifa ya Afrika lilifanyika mjini Khartoum, Sudan. Hakukuwa na mechi za kufuzu katika shindano hili , kwani uwanja ulikuwa na mataifa manne ambao ndio wanzilishi wa CAF (Sudan, Misri, Ethiopia, na Afrika ya Kusini). Kukataa kwa Afrika ya Kusini kupeleka kikosi chenye wachezaji wa rangi tofauti katika ushindani kulisababisha wao kuadhibiwa na Ethiopia iliweza kufuzu katika fainali, Kutokana na tukio hilo mechi mbili ndizo zilizochezwa na Misri kuwa bingwa wa kwanza katika bara baada ya kushinda Sudan katika nusu fainali na Ethiopia katika fainali. Miaka miwili baadaye, Misri ndiyo ilikuwa mwenyeji wa pili wa ANC mjini Cairo ambapo timu zile tatu ndizo zilishiriki .Kama mwenyeji na bingwa tetezi Misri iliweza kushinda baada ya kuwalaza sudan katika fainali.

Shindano hili lilienea na kuwa na timu tisa ambazo zilishiriki. Shindano hili la tatu la ANC mwaka 1962 lilikuwa mjini Addis Ababa, na kwa mara ya kwanza kulikuwa na mechi za kufuzu ambapo timu nne zilifuzu kupigania ubingwa. Ethiopia kama mwenyeji Misri kama bingwa mtetezi zilipata fursa ya kufaulu mara moja, na kuungwa na Nigeria na Tunisia katika timu nne za mwisho zilizo waania ubingwa. Misri iliweza kucheza fainali kwa mara ya tatu lakini Ethiopia waliwezakushinda, baada ya kupiga Tunisia katika nusu fainali nakulaza Misri katika muda wa ziada.

Katika mwaka 1963, Ghana ilishiriki kwa mara ya kwanza katika shindano hili na iliweza kunyakua ushindi baada ya kuilaza Sudan katika fainali, iliweza kunyakuwa ubingwa miaka miwili baadaye katika Tunisia ikisawazisha na Misri kama bingwa wa misimu miwili na kikosi ambacho kilikuwa na wachezaji wawili tu kutoka timu ya 1963.

katika shindano la 1968 ilibidi mpango wa mchuano huo ubadilike na kuongeza hadi timu 8 zitakazo faulu kati ya timu 22 zilizofaulu katika raundi ya hapo awali. Timu zilizofaulu ziligawanyishwa katika makundi mawili kila kundi likiwa na timu nne ambazo zilicheza michezo ya mizunguko ambapo timu mbili bora zaidi katika kila kundi zilifaulu katika nusu fainali.Mfumo huu uliendelea kutumika katika fainali hadi mwaka wa 1992. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliweza kushinda baada ya kuwachapa Ghana. Kuanzia mwaka wa 1968 shindano hili limekuwa likitendeka baada ya miaka miwili katika miaka iliyo sawa. Mchezaji wa mbele wa Ivory Coast, Laurent Pokou aliongoza kwa mabao katika michuano ya 1968 na 1970 kwa mabao sita mwaka wa 1968 na mabao nane katika mwaka wa 1970 na kuwa na mabao 14 kwa jumla na kushikilia rekodi kwa muda hadi 2008. Shindano hili liliweza kuonyehwa katika runinga mara ya kwanza mwaka wa 1970 likiwa nchini Sudan, ambayo iliweza kuchukua taji baada ya kuwashinda Ghana iliyokuwa ikicheza fainaili ya nne mfululizo.

Kati ya mwaka 1970-1980 mataifa sita mbalimbali yaliweza kushinda : Sudan, Kongo-Brazzaville, Zaire, Moroko, Ghana, na Nigeria. Zaire ilishinda mara ya pili katika mwaka wa 1974 ilishinda mara ya kwanza kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kupambana na Zambia katika fainali. Kwa muda hadi sasa katika historia ya ushindani, hii ndio mechi ya kipekee ambayo imerudiwa baada ya timu hizo mbili kutoka sare 2-2 baada ya muda wa ziada. Finali hii ilichezwa siku mbili baadaye na Zaire kuibuka washindi kwa 2-0. Mchezaji wa mbele wa Zaire , Mulamba Ndaye alifunga bao zote nne za mechi hizo mbili: pia alikuwa alishikilia usukani kwa kuwa na mabao tisa katika msimu huo na kuweka rekodi ya mechi ya kibnafsi hadi wa leo. Miezi mitatu awali, Zaire ilikuwa taifa la kwanza la Afrika weusi kufuzu katika FIFA World Cup. Morocco iliweza kuchukua ushindi kwa mara yao ya kwanza katika ANC mwaka wa 1976 nchini Ethiopia na Ghana ilichukua ushindi mara ya tatu mwaka wa 1978,Katika mawka wa 1980 shindano hili lilifanyika Nigeria ambapo timu ya taifa ya Nigeria ililaza Algeria na kunyakuwa ushindi mara ya kwanza.

Tangu 1962 kumekuwa na michuano ya kufuzu katika fainali. Kutoka 1962-1990 michuano hii ilikuwa na mechi za kurudiwa, na idadi ya raundi ilitegemea idadi ya timu zinazoshiriki Kuanzia 1994 kuendelea timu ambazo zina azma ya kufuzu hugawanywa katika makundi na kucheza na kila timu katika kundi iliyowekwa Mpaka mwaka wa 2006 ambako timu ya nchi ambapo shindano hili litafanyika na mabingwa tetezi zilifaulupapo Kwanzia mwaka wa 2008 timu itakayo fanya shindano hili ndio wanafuzu papo hapo.Fomati ya kufuzu katika shinano hili imekuwa ikibadilikabadilika .Kwanzia mwaka wa 2008 timu 11 ndizo zinazofuzu katika fainali ambazo zinagawanya katika makundi ambayo yana timu nne na moja timu tatu. Timu zinazoshinda katika kundi ndizo zinafaulu na timu tatu zingine ambazo zina rekodi nzuri.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement