Katika maisha kunavitu viwili, Rekodi na Heshima Ni vitu viwili vinavyoendana sana lakini usipovipambania na kuvilinda mara baada ya kuvipata ni lazima ukubali kuwa utabeba viwili ambavyo vitakuwa kinyume chake.

Na ndicho ninachokiona kwa wawakilishi wetu wanchi kunako michuano ya Kimataifa Simba SC ambao watavaana na Al Ahly katika mchezo wa marudiano Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Mapambano hayajawahi kukatiwa tamaa kabla haujaimaliza vita yenyewe.

Ni Heshima dhidi ya Rekodi katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba wakiisaka Heshima huku Al Ahly wakiisaka Rekodi kunako michuano hiyo.

Simba SC wapo wameshatua kwenye Ardhi ya ugenini Nchi ya Misri, wakiwa wameuacha Uwanja wa nyumbani wa Benjamini Mkapa ambao umekuwa ukiwapa rekodi Bora lakini katika mchezo wao wa kwanza ikiwa ni tofauti wakipoteza dhidi ya Al Ahly mchezo wa kwanza Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kikawaida huwa tunamsemo unaosema, Hata mbabe anambabe wake pia.

Al Ahly ni Bingwa mtetezi wa Michuano hii, lakini haliweki hofu mioyoni mwa wapinzani wao kwa maana ya Simba SC kwamaana hata wao wanajiamini katika upambanaji na itakuwa sio mara ya kwanza kumvua bingwa mtetezi Ubingwa wake iwapo watafanikiwa kupata matokeo mazuri ya ugenini.

Kwa miaka ya hivi karibuni timu hizi mbili zimekutana mara saba kwenye michuano ya CAF, ambapo Simba SC wakiwa wameshinda mara mbili na kupoteza mchezo mmoja wakiwa nyumbani huku wakipoteza mechi mbili za ugenini, Al Ahly wakishinda mechi mbili za nyumbani na kupoteza mbili ugenini ambapo timu zote zikipata sare katika michezo ya hivi karibuni.

Mechi hizo ni zile za Michuano mipya ya African Football League kwamaana ya AFL ambapo mchezo wa kwanza uliopigwa kwa mkapa Oktoba 30 mwaka jana ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2, Mechi ya Marudiano ikapigwa Cairo nchini Misri sna kumalizka kwa sare ya bao 1-1.

Kutokana na Rekodo hizo, kila timu inatamani kusaka Heshima ambapo Simba SC itataka kushinda ili kuweza kutoa furaha kwa watanzania kwa kufuzu Nusu Fainali huku Al Ahly wao wakihakikisha pia wanashinda ili kufuzu Nusu Fainali na hatimaye Fainali ili iweze kutetea Ubingwa wao.

Simba SC inataka heshima ya kuvuka Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu huu baada ya kujikuta wakiishia hapo mara nne katika misimu mitano iliyopita.

Pia Al Ahly itataka heshima ya kuendelea kutawala soka la Afrika kwa kucuka hatua hiyo na kutwaa taji hilo iliyotwaa kwa mara nyingi zaidi kwenye Historia ikifanya hivyo mara 11.

Wakati Simba SC inamtengeneza zaidi Saido Ntibazonkiza ambaye amehusika kwenye mabao manne ya michuano hii msimu huu, Al Ahly wao itakuwa ikitegemea ubora wa Hussein El Shahat ambaye amehusika kwenye mabao matatu.

Simba SC kwao ni mechi inayohitaji kujitoa zaidi kwaajili ya kuwaonyesha waliowakatia tamaa kuwa hata aliyeanguka anaweza kusimama na kusonga mbele kwa kufika mbali zaidi ya anavyodhaniwa.

Na hapa ndipo tunapoona Dhahiri ya kuwa, Heshima ikibebwa kwa kuipambania bila kuilinda basi tambua wazi utabeba mazoea na dharau na ukikubali kuibeba Rekodi basi lazima ukubali kuyabeba maumivu na kubezwa.

Simba SC watavaana na Al Ahly katika mchezo wa mkondo wa Pili ambapo mshindi wa jumla atatinga hatua ya Nusu Fainali.

Al Ahly wao wameshatanguliza mguu mmoja baada ya ushindi wa mchezo wa mkondo wa kwanza Dimba la Mkapa akifanikiwa kuokota ushindi kwa mwenyeji wake, Ni zamu ya Simba SC kuokota ushindi wa ugenini japo watu wengi wanatazama kama jambo gumu na lisilowezekana lakini tukumbuke chini ya jua hakuna linaloshindikana ukiweka Nia na Juhudi ambazo zinadhamira ya kukufikisha kwenye mafanikio makubwa.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement