Ndio lugha rahisi zaidi ya kumuelezea Mudathir Yahya Abbas.

Kwa sasa yeye ndio box to box midfielder bora zaidi kwenye NBC Premier League kutokana na takwimu zake.

Je box to box midfielder ana tabia/sifa zipi? Au ana majukumu gani kwenye timu?

Kwanza maana ya (B2BM) ni kiungo anayetoa uwiano mzuri kwenye ma box yote mawili ndani ya kiwanja, kwenye box la kuzuia na kwenye box la kushambulia.

Kiufupi majukumu yake ni kuwa kwenye maeneo yote mawili kutegemeana na mazingira ya mpira upo wapi.

Mpira ukiwa kwenye eneo lake la kuzuia basi tunategemea kumuona akiongeza idadi ya wachezaji wanaouzia Ili kuipa timu muundo mzuri wa uzuiaji lakini kama mpira upo kwenye box la mpinzani basi anapaswa kuongeza idadi ya wachezaji wanaoshambulia box la mpinzani.

Kwa maelezo yote mawili hapa Mudhathir Yahya anaingia vizuri na anatimiza vyema majukumu yake.

Simply Mudhathir Yahya yupo kwenye

1. Defensive play

2. Attacking play.

Kwa majukumu haya tegemea kumuona Mudhathir muda mwingi akiloa jasho kwasababu anatembea eneo kubwa la kiwanja.

Kufunga magoli mfululizo inakupa picha kwamba analitendea haki box la juu(, offensive play).

Halafu Kuna sifa nyingine anayo akiwa kwenye nusu ya juu kuelekea final third.

Huwa ana act AS THIRD MAN RUNNER.

THIRD MAN RUNNER ni nani? Ni mchezaji wa tatu ambaye hana mpira anayefanya mikimbio baada ya kuona wachezaji wawili wa timu yake wakiwa wana pasiana,lengo lake ni nini?

Lengo lake ni kuona ule mpira wa mwisho wa wale wachezaji wawili,yule wa mwisho kupasiwa akipewa hiyo mali ataipiga ndani ya box ambapo ndio hapo hapo Mudhathir alipo/anapofanya mikimbio akiiba nafasi iliyochwa wazi na walinzi wa timu pinzani.

Amefunga magoli kama mawili kwa kutumia concept hii ya THIRD MAN RUNNER.

Kiufupi tu, Mudhathir yupo kwenye kiwango cha juu na anafurahia kucheza na kufunga magoli kila baada ya mechi.

Keep shinning brother Mudhathir Yahya Abas.


IMEANDALIWA NA: FARAJI MUSTAPHA

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement