"Mara ya kwanza wakati nakutana na Ronaldo kwenye mechi nilikuwa naitumikia timu ya Parma. Dakika chache baada ya mechi kuanza, nilikutana nae macho kwa macho akiwa anafanya mikimbio huku anakokota mpira kwa kasi.

Sikuwahi kuona vitu kama vile kwa kipindi cha nyuma kwenye maisha yangu ya kucheza mpira (uwezo mkubwa wa Ronaldo). Akiwa anakokota mpira akawa analisogelea goli letu. nikajaribu kumkwatua lakini sikumpata, haraka nikamgeukia Fabio Cannavaro nikambwatukia muweke chini huyo, Cannavaro alilazimika kumkwatua Ronaldo bahati nzuri Refa alimuonya tu Cannavaro mechi ikaendelea.

Baada ya dakika kadhaa Ronaldo alikuja tena mbele yangu akiwa ana kokota mpira kwa kasi ile ile, sikuwa na cha kufanya maana alinipita na sikuweza kumzuia. Cannavaro akaniangalia na akaniambia. "Lily, tutamaliza mechi tukiwa wachezaji 9 usiku wa leo kama tusipokuwa makini, tunawezaje kuzuia hii hali?.

Kumbe wakati tunaongea haya yote, Ronaldo alikuwa anatusikiliza na ghafla aligeuka na kutufuata akatuambia, "Samahani, leo nasifiwa sana kuliko uwezo wangu"

Kwa maneno yale tulijiona kama watoto ambao hawana msaada, hayo ni maneno ya nguli Lilian Thuram akimuelezea Ronaldo de Lima jinsi ambavyo alikuwa bora pindi awapo uwanjani.

Dunia inakosa kabisa aina ya washambuliaji kama hawa waliowahi kutisha miaka ya nyuma, wanazungumzwa wachezaji wengi wa zamani akiwemo Pelle na Maradona kama ni moja ya wachezaji waliowahi kufanya vizuri kwenye medani ya kabumbu ulimwenguni, lakini jina la Ronaldo lina zungumzwa kwa herufi kubwa sana na wapenda soka kutokana na uwezo aliokuwa nao enzi zake.

Kasi ndani ya uwanja, maarifa, nguvu, uwezo wa kufunga magoli kwa kupiga mawe tena kwa kutumia miguu yote miwili kwa ufasaha, maono awapo uwanjani, ni moja ya vitu vilivyokuwa vinamtofautisha kwa kiasi kikubwa Ronaldo na washambuliaji wengine.

Familia ya soka na mitaa yote kwa ujumla bado tunaendelea kutukuza na kuhusudu uwezo wa Ronaldo kutokana na kile alichokuwa anakifanya enzi zake.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement