Tarehe 11 Mwezi wa 7 Mwaka 2021 baada ya vikosi kutoka kwa Timu za Taifa mbili za England na Italy kwenye Mchezo wa Fainali ya Euro 2020 pale kwa Malkia WEMBLEY STADIUM .Basi kila Mpenzi wa soka Mkono wake ulikuwa kinywani huku akiangalia Mabeki wawili wa Timu ya Taifa ya Italia.

Kila mtu alijiuliza kijana kama Mason Mount Bingwa wa Champions League na uhodari wake anaenda kukutana na Vikongwe?, Harry Kane namba 9 hatari Duniani anaenda kukutana na Vikongwe.


Maneno yalikuwa mengi kwa wadau wa soka baada tu ya vikosi kutoka maana kwenye ukuta wa Italy ya Robert Mancini walisimama Giorgio Chiellini na Leonardo Bonnuci ambaye sio DiCaprio au Leonardo wa bila ya D mbili huwezi kuelewa.

Wakongwe ambao kuchukua Sheria mkononi washaachaga zamani na sio michongo yao kabisa na Tabia za Umbea sio zao maana washakuwa wakongwe .

Lakini Bonnuci na Chiellini waliacha Hadithi kwenye EURO huku wakiondoka na Ndoo mbele ya vivulana vya Gareth Southgate na sera yao ya IT'S COMING HOME, Leonardo Bonnuci aliondoka na Historia yake ya kuwa Mchezaji Mkongwe zaidi kufunga bao kwenye fainali ya EURO, Hakuna aliyeamini kwamba Vikongwe wangeifanya ile hadithi ya BRICK WALL kuwa yakweli dhidi ya Vijana wa Kingereza lakini Wahenga walisema " Kila kijiji hakikosi wazee na Wazee hao walikuwa ni Bonnuci na Chiellini.


Pindi Dunia ikiwa kwenye fujo za Nemanja Vidic na Rio Ferdinand , Puyol na Pique na Sergio Ramos na Pepe kama pacha bora kwa vizazi hivi vya Yope basi mimi nakuja na pacha ya Bonnuci na Chiellini. 

Ipo Underrated sana hii pacha labda huenda ni kisa haina Champions League lakini vipi kama Cristiano Ronaldo asingezaliwa ? Huenda zingekuwa kabatini hizo Champions League.Kama Dunia ipo kwa Marco Reus basi isisahau kuwa haikuwahi kukaa nyuma ya Bonnuci na Chiellini kwenye Dimba la CARDIFF.

Kama Uaminifu ni kigezo cha kukaa nyuma ya Reus basi tusisahau Martina Maccari alivyomwaga Mchele kwenye kuku wengi baada ya kusema "I loved you and Hated you " Bibie Martina aliwaambia Juventus kwamba Niliwapenda na kuwachukia Sababu tu Mumewe Leonardo Bonnuci alikuwa bize na Juventus kuliko Mke wake.

Kwenye upepo Hidaya wa Ramos na Pepe basi Bonnuci na Chiellini walikuwepo , kitaa hakijawasahau , kitaa bado kimeandika majina yao kwenye waliobora kwa kizazi hichi cha Komasava.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement