Baada ya kisanga cha sare kati ya Liverpool na Manchester City kwenye uwanja wa Anfield siku ya Jumapili, sasa ni wakati mzuri wa kutathmini mbio za kusisimua za kuwania taji la Ligi Kuu ya Uingereza huku zikiwa zimesalia mechi 10.

Kwa mara ya kwanza tangu 2014, pointi moja pekee ndio inatenganisha timu tatu za juu baada ya michezo 28 iliyochezwa.

Timu tatu za juu hazitocheza ligi kuu kwa muda wa wiki tatu - kwa sababu ya robo fainali ya Kombe la FA na mapumziko ya kimataifa. Watakaporejea Liverpool itacheza na Brighton na Manchester City itaikaribisha Arsenal Jumapili Machi 31.

Kikosi cha Pep Guardiola cha City kinatisha huku kikipania kuweka rekodi ya ligi kuu ya Uingereza ya kutwaa mataji manne mfululizo. Tangu walipofungwa 1-0 na Aston Villa mwezi Disemba - wameshinda mara 10 katika mechi 13 za ligi.

Kwa upande wa Liverpool, kipigo cha 3-1 kutoka kwa Arsenal Februari 4 kinasalia kuwa kipigo pekee ndani ya ligi katika mechi zao tisa hadi sasa toka 2024.

Kikosi cha Liverpool chini ya Jurgen Klopp bado kina safari ya kwenda katika uwanja wa Goodison Park kwa dabi ya Merseyside dhidi ya Everton.

Kwa upande wa Arsenal, ingawa wikiendi hii wamemaliza wakiwa kileleni mwa jedwali, Simon Gleave, mchambuzi wa soka anasema.

Ni mbio za farasi wawili, City na Liverpool watakuwa mstari wa mbele wa kinyang’anyiro huku Arsenal ama washika bunduki, itakuwa na ratiba ngumu zaidi.

"Arsenal wamebakiwa na mechi sita katika Premier League, tano kati ya hizo ni ugenini. Manchester City wana mechi sita, nne kati ya hizo ni nyumbani. Liverpool pia wamebakisha mechi sita na tatu kati ya hizo wako nyumbani,"

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement