Jude Bellingham amefunga mara 10 katika mechi 10 akiwa na Real Madrid tangu ahamie Madrid Uhispania. Pia ametoa pasi tatu za mabao kwa Los Blancos msimu huu na tayari amefananishwa na mchezaji wa Ufaransa na kocha mkuu wa zamani wa Madrid Zinedine Zidane.

Wakati Madrid ilipomsaini Bellingham, mwandishi wa habari Julio César Iglesias alitabiri kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 angekuwa mchezaji bora wa muda wote katika klabu hiyo, akisema kwamba kiungo huyo wa zamani wa Birmingham City na Borussia Dortmund atakuwa "mchezaji bora zaidi wa klabu tangu Alfredo Di Stéfano" .

Di Stéfano alifunga mechi yake ya kwanza ya Real Madrid na kutikisa nyavu mara 11 alipokuwa amecheza mechi 10 akiwa na Real Madrid, nambari sawa na za Bellingham.

Julio César Iglesias anasema, kwamba Bellingham anaweza kuwa bora Santiago Bernabéu katika miaka ijayo.

Bellingham yuko katika mazingira ambayo yamemruhusu kuanza na anacheza nafasi ya juu zaidi chini ya Carlo Ancelotti kuliko wengi walivyotarajia.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement