Unahitaji kuwa na shilling 450 za kitanzania, kutoka katikati ya Jiji la Buenos Aires au Kariakoo ya Buenos mpaka San Fernando de la Buena Vista mitaa hii ni kama Tandale kwa Tumbo ya Dar Es Salaam, mitaa hii imemlea RiqueBaller Juan. 

Jioni moja katikati ya miaka ya 90 Kocha wa Boca Juniors, Bwana Carlos Salvador Bilardo alitembelea mitaa hii mitakatifu kabisa ya soka, ghafla macho yake yalitua kwa Juan mwenye miaka 16 tu na namba 10 mgongoni, akitandaza mpira anavyotaka yeye, juu ya vumbi na tambaa la Unahodha

Bilardo alisogea pembeni na kumuuliza kijana mmoja "Quien es ese" kijana alimjibu "Es decir Diego Maradona" Jamaa alichoka sana, yani aliuliza yule nani, ila kijana akamwambia yule ni Diego Maradona, yani kuna mitaa ya Argentina ina Maradona mwingine uwanjani na anakipiga. 


Ilikua mchakato wa haraka sana, kwa Boca Juniors kupambana kuipata saini yake kutokea Argentino Junios, na pale La Bombonela ilikua balaa sana, walimpa jezi na akiwa na miaka 18 tu, moto uliwaka sana uwanjani, alicheza namba 10, akicheza kama hataki ila ufundi mwingi mno. 

Miaka ya 2000 wale Barcelona hawakutaka kabisa kumuelewa kocha wao Luis Van Gaal, alikataa usajili wa Juan ila bodi ilimpinga, unamuachaje Maestro kama yule, wakamleta Barca ila LVG akauita usajili wa kisiasa na kuamua kumtia benchi. 

Maradona wa San Fernando alikula sana mkeka pale Nou Camp, ila kila akipewa namba anachezeshwa winga ila alikua bado fundi mno, anatokea pembeni na kijiji chake na kutupia sana, akapewa Mwenyekiti wa Kijiji cha Mawinga wote Spain. 

Maisha yake yalitakata baada ya kwenda kwa Nyambizi wa njano, Villareal ndipo hapo miguu ya almasi na akili ya kioo ikafahamika duniani kote, alichezeshwa kama Central Midfielder, alikuwa na Orchestra moves yani miondoko kama vinanda vya Tuddy Thomas anafunga kutokea kati na kuchezesha mno. 

Inaaminika ni namba 10 ya mwisho asili duniani, mikononi mwake ana tuzo za mchezaji bora wa mwaka Argentina mara nne, alizaliwa tarehe 24-06-1978 siku moja kabla Argentina ajabeba kombe la dunia, FALTA MAGICIA, FALTA ROMAN. 

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement