Dakika 3 na sekunde 31 sauti ya Mjeshi Harmonize na Badgirl Spice, sijui ni kwanini ila huwa sitamani ngoma ya Miss Bantu iishe.

Ni katikati ya marehemu Christian Atsu, miguu ya fundi Issama Mpeko na Mido Wakaso Mubarak ulipigwa mpira mrefu kutoka alipo golikipa wa Congo Ley Matampi kisha ukawavuka ndugu wawili Jordan na Andre Ayew, tayari Ball Boy mmoja alishajivuta kuuokota ule mpira unaoelekea kutoka nje Chancel Mbeba na kasi yake yote alishakata tamaa mpira ulikuwa mrefu sana Wakati Line One akijiandaa kuamuru mpira wa kurushwa kuelekea lango la Congo, 

zilisikika sauti za shangwe za wendawazimu na vichaa wa soka kutoka kwenye jukwaa moja la VIP pale dimbani Stade Oyem, sijui nini kiliendelea ila nachokumbuka tayari mpira ulikuwa umetulia chini ya mguu wa kushoto wa Joyce Lomalisa Mutambala.

Afcon 2017 Congo dhidi ya Ghana, bahati mbaya njozi yangu iliishia pale ila sikutamani iishe Asubuhi moja ya joto la Dar na umbea wa Insta nilisikia Yanga wamemsajili Joyce Lomalisa kutoka Inter De Luanda ya Angola, mitaa na waswahili wa Kariakoo walidai huyu ni moja kati za sajili za kitapeli Mchezaji anaitwa Joyce? 

Mchezaji kachafukwa tatoo mwili mzima? 

Nami sikutia neno lolote kwa huyu mzaliwa wa June 18 mwaka 1993 pale Congo ila nilitaka kujua kama ndiye yule aliyenifanya nimtukane tusi zito Mjomba aliyeniamsha usiku wa ndoto tamu 

Yes ndiye yule mtu wa ndoto nzuri, nikawaambia "Mbrazil amezaliwa Congo" mtu mwenye udambwi wake, positional awareness ni kama Marcelo akiover lup na kusprint ananikumbusha ubavu wa Ashley Cole sio Paollo Maldin huyu ni Joyce Lomalisa.

Siku hizi wanamwita Waziri wa maji, ila huku Banda Umiza tunamwita Joyce Lomalinho 

Kwa kuwa watanzania sio wapenzi wa mpira burudani hawawezi kumuelewa Joyce Limolisa mutambala kwa kuwa yeye ni mtaalamu wa mpira burudani.

Anatoa burudani kali ndani ya uwanja kuliko hata nyimbo za Mario au Lavalava wakiwa stejini 

Tusubiri tuone mwisho mwa ufalme wake utakuwa lini lakini wananchi wamafanikiwa kuona kipaji maridhawa kwenye timu yao kikitoka kwenye ardhi safi ya soka iliotukuka 

Ardhi ambayo imezalisha mastaa wengi bora duniani na wenye mvuto ingawa Lomolisa wa AFCON 2017 alikuwa hatari zaidi

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement