AFCON2023, ni moja ya michuano ambayo imeingia katika historia kubwa Zaidi katika historia ya mashindano haya.

Ni matokeo yasiyokuwa yakutarajiwa, kutoka hatua ya makundi mpaka mtoano katika michuano hiyo iliyoanza kutimua vumbi Januari 13 mwaka huu na sasa ikiendelea nchini Ivory Coast.

Licha ya kuondolewa kwa vigogo wa soka Barani Afrika, kama Algeria, Misri, Morocco, Tunisia, Cameroon nahata Bingwa mtetezi wa michuano hiyo, Timu ya Taifa ya Senegal, Mataifa ambayo yameorodheshwa katika nafasi 10 za juu barani Afrika kwa viwango vya FIFA.

Maboresho ya zawadi za mabingwa pia yameweka historia nyingine kwani Bingwa atapokea kiasi cha Dola Milioni saba sawa na Shilingi za Kitanzania Bilioni 17.5 ambalo ni ongezeko la asilimia 40 kutoka kwenye michuano iliyopita jambo lililoleta ushindani Zaidi.

Kwa nini tunasema historia imebadilishwa au kuvunjwa? Hii inajidhihirisha wazi waliokuwa wakitazamwa Zaidi ni wale ambao wameshawahi kuchukua Ubingwa wa Michuano hii.

Mabingwa wa Kihistoria, Mafarao Timu ya taifa ya Misri wao wanajumla ya Makombe saba, na licha ya makombe hayo saba ya Ubingwa wa AFCON kwa msimu huu wa AFCON2023 umekuwa na bahati mbaya kwao baada ya kuondolewa na DR Congo.

Cameroon wao wanamakombe matano ya Ubingwa wa AFCON, wameondolewa na Timu ya Taifa ya Nigeria katika michuano hii ya AFCON2023, Mchezaji na Nahodha wa Timu ya Taifa hili la Cameroon ndiye anayeshikilia kiatu vha mfungaji bora wa msimu uliopita wa michuano hii, Vincent Aboubakary.

Ghana wanamiliki makombe manne, msimu huu wa AFCON2023 kwao umekuwa mbaya kwani wao waliondolewa katika hatua ya makundi.

Nigeria wao wanamakombe matatu ya ubingwa wa michuano hii, wao bado wanasafari ya Robo Fainali, wakitazamwa kama mabingwa wa michuano hiyo kwa msimu huu.

DR Congo, wao wanamiliki makombe mawili, ubora wao waliouonyesha kwa kuangalia mapungufu sambamba na kuyarekebisha ndio umewafikisha walipo, mpaka wamefika hatua ya Robo Fainali hawajashinda mechi yoyote Zaidi ya sare na kisha Mikwaju ya Penati.

Wenyeji wa Michuano ya AFCON2023, Timu ya Taifa ya Ivory Coast, wao wanajumla ya makombe mawili pia, wamefuzu kutoka hatua ya Makundi kama Best Looser, wengi walipoteza matumaini nao baada ya kupokea kipigo cha bao 4-0 kutoka kwa Guinea ya Ikweta, lakini hakuna aliyeamini kama wangeweza kuwavua Ubingwa, Mabingwa watetezi wa Michuano hii, Timu ya Taifa ya Senegal.

Afrika Kusini wao wanakombe Moja, na iwapo watafanikiwa kuchukua la msimu huu wa AFCON basi watakuwa wameongeza idadi ya maombe na kufukisha mawili, wao wapo robo Fainali wakiwatoa vigogo wa soka, Timu ya taifa ya Morocco katika hatua ya 16 bora.

Simba wa Milima ya Teranga, Timu ya Taifa ya Senegal, Mabingwa watetezi wa michuano hii lakini wahakuamini kwa kilichowakuta, walipoteza mbele ya mwenyeji, Ivory Coast na hawana chao tena kwa sasa.

Algeria, wanamiliki Makombe mawili, msimu huu pia umekuwa wa bahati mwaya kwao kama ilivyokuwa kwa Ghana, wao pia waliondolewa katika hatua ya Makundi.

Morocco, Tunisia na Zambia wote wanamiliki kombe la Ubingwa moja kwa kila mmoja, Mataifa haya pia hayakuwa na bahati katika mashindano haya yenye historia kubwa, wameondolewa kweye mashindano ya msimu huu.

Sudan na Ehiopia wao pia wanakombe moja kwa kila Taifa, lakini hawapo kwenye Fainali hizi za Mataifa ya Afrika, AFCON2023.

Ukimtazama mwenyeji wa Michuano hii ambaye aliingia kama Best Looser, japo ni Taifa lenye ubora kunako soka lakini halikuwekewa matarajio makubwa kama lingeweza kufikia hatua ilipo sasa.

Waliobakia kwa sasa ndio wenye dhamana ya kuhakikisha wanapambana na kupatikana Bingwa wa michuano hiyo.

Ni hatua ya Robo Fainali ambayo itawakutanisha Blue Sharks Timu ya Taifa ya Cape Verde dhidi ya Afrika Kusini, Mali kibaruani dhidi ya The Elephant kwa maana ya wenyeji wa michuano, Timu ya Taifa ya Ivory Coast, The Leopards, DR Congo wao watakutana na The Syli National, Timu ya Taifa ya Guinea huku Super Eagles, Timu ya Taifa ya Nigeria wakikutana na Angola, The Palancas Negras.

Mwenyeji wa michuano hiyo, Timu ya Taifa ya Ivory Coast ambao hawakupewa kipaumbele mara baada ya kutokuwa na matokeo ya kuridhisha katika hatua ya makundi Michuano ya AFCON 2023.

Japo walifuzu hatua ya 16 bora kama Best Looser, ila shirikisho la Mpira wa Miguu nchini humo chini ya Rais wake Yacine Idriss Diallo iimfungashia virago kocha Raia wa Ufaransa Jean Louis Gasset ambaye alianza kazi ya kukinoa kikosi hicho mwaka 2022.

IVORY COAST wametinga hatua ya Robo Fainali wakiwatoa mabigwa watetezi wa michuano hiyo, Timu ya Taifa ya Senegal kwa mikwaju ya Penati 5-4 baada ya mchezo kumalizika dakika 102 ubao ukisoma 1-1.

Mali: wao wamefanikiwa kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza ikiwa imepita miaka 10 waliichapa Burkina Faso bao 2-1.

Ulinzi mkali wa Mali ulipunguza nafasi za wapinzani wao Bao la dakika za lala salama lililokataliwa kwa Burkina Faso.

Wakati wengi wakiwa hawana imani na uwezo wa Ivory Coast mbele ya Senegal lakini tumeona mbavyo wamebadilika mno na kuwanyanyasa vya kutosha timu ya Taifa ya Senegal huu ikionyesha wazi kuwa yote ni uwepo wa Kocha mpya ambaye ni mchezaji wa zamani Emerse Fae ambaye amepewa mkataba wa muda.

CAPE VERDE ni mojawapo ya timu zilizoshangaza wengi katika michuano hii baada ya kumaliza bila kufungwa kileleni mwa Kundi B mbele ya Misri na Ghana, walikuwa wa pili bora kwa muda mwingi wa kipindi cha kwanza, lakini walimaliza kwa nguvu na kujihakikishia kupita

AFRIKA KUSINI wamewazamisha Vigogo wa soka Barani Afrika na kwenda hatua ya Robo Fainali.

Kweye kikosi cha Bafana Bafana, wachezaji asilimia kubwa walitoka Ligi ya ndani kunako Klabu ya Mamelodi Sundowns ambapo ilikuwa na jumla ya wachezaji nane ambao ndio walioanza katika kikosi cha kwanza.

Morocco hawakuwa na mchezaji yeyote anayecheza Ligi ya ndani ya Afrika katika kikosi chao cha kwanza.

Kati ya wachezaji 11 wa kikosi cha kwanza cha Morocco kilikuwa na wachezaji tisa wanaocheza katika Ligi tano bora duniani (EPL, La Liga, Bundesliga, Ligue 1 na Serie A) na wachezaji wawili wanacheza Ligi ya Saudi Arabia.

Evidence Makgopa na Teboho Mokoena walionekana mwiba mchungu kwa Simba wa Milima ya Atlas, Morocco walipata nafasi ya kusawazisha, lakini Achraf Hakimi alikosa penalty, Sofyan Amrabat alitolewa kwa kadi nyekundu dakika za lala salama.

ANGOLA wakawamewafedhehesha Namibia ,Brave Warriors katika derby ya COSAFA mabao 3-0 na kufuzu kwa robo fainali ya kombe la AFCON.

Angola wanafuzu kwa robo fainali ya AFCON kwa mara ya tatu na ya kwanza tangu mwaka 2010 wakiwa wenyeji.

Guinea: Timu ya kocha Sebastien Desabre itaelekea Abidjan kwa mtanange wa robo fainali dhidi ya Guinea, ambayo iliichapa Guinea ya Ikweta 1 – 0 , ni mechi ambayo Guinea ya Ikweta hawataisahau kwani Wakati mechi ilionekana kuwa inaingia muda wa nyongeza, Mohamed Bayo alifunga bao katika dakika ya nane ya muda wa majeruhi na kukivuruga kabisa kikosi cha Guinea ya Ikweta.

Ulikuwa ushindi wa kihistoria kwa Guinea, ambao hawajahi kushinda mechi ya mtoano ya AFCON.

kocha wa Guinea Kaba Diawara, alidondosha machozi ya furaha.

Wakati huo huo, Guinea ya Ikweta, ambayo ilishuhudia mchezaji wake wa kiungo cha kati Federico Bikoro akitimuliwa uwanjani katika dakika ya 55, najua ulijiuliza ni nini kingetokea kama nahodha wao Emilio Nsue asingepoteza mkwaju wa penalti katikati ya kipindi cha pili.

Niwajuze tu, Kutoka kundi A zilizofuzu Robo Fainali ni Ivory Caost na Nigeria, Kundi B likitoa ttimu kutoka Ghana pekee, Kundi C pia wakibakia Guinea pekee, Kundi D wakipenya Angola huku Kundi E wakionekana Mali na Afrika Kusini na Kundi F likiwakilishwa na DR Congo 

Ni mwenyeji pekee, Timu ya Taifa ya Ivory Coast ambao walimtimua Kocha na sasa wapo hatua ya Robo Fainali ya Michuano hii mikubwa kabisa Barani Afrika, AFCON2023.

Tuendelee kusubiri na kuona, ni nani atapenya kwenda Nusu Fainali ya Michuano hii.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement