Linex Sunday Mjeda, Haliwezi kuwa jina geni kwenye kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva moja kati ya Ma Vocalist wakali sana, Ni vile tu kama muda unamtenga. 

Masikio yetu yameshasikiliza ngoma zake kali, Kuanzia Mama Halima,Aifola,Salima. Jamaa ni muandishi mzuri sana. Umewahi kuipa sikio Wema Kwa Ubaya? 

Na ukasikiliza yale mashairi Achana na ule unyama kwenye chorus ya Kigoma All Stars, Kwangu bado sijamuona Linex wa Moyo Wa Subira.

 Moyo wa Subira Linex Sunday Mjeda anamzungumzia binti mzuri wa ndoto zake ambaye wameachana sasa anaomba warudiane, Linex akalia sana mule ndani akihitaji ubavu wake urudi. 

Hivi Philippe Coutinho na Linex kuna uhusiano gani?

 Kwenye moyo wa subira Linex anasema "Laiti kama angeweza azirudishe siku nyuma ili apate msamaha' Lakini alishachelewa.

Ni ghalfa kwenye mashairi ya Linex Namkumbuka Little Magician Ni yule Coutinho wa Anfield, Ni yule fundi wa Brazil ndani ya Liverpool alijua kufanya kazi kweli kama kiungo mshambuliaji.

Mauricio Pochettino aliwahi kusema Coutinho he has a special magic in his feet, Wakati yupo Inter Milan Rafael Benitez alisema Coutinho is the future of Inter Milan pale Rio De Janeiro walikuwa wakimfananisha na fundi Zico.

Coutinho alifanya kila kitu ndani ya Liverpool Dunia haikuwa na Mwanadamu wa kumzidi Coutinho kwa kufunga mabao kwa mtindo wa Curve, Makipa wa EPL waliumia sana. 

Ogopa sana ndoto, Ndoto za Coutinho zilikuwa Camp Nou, akaamua kuzifuata, Na Wacatalunya wakaamini nafasi ya Andres Iniesta imepata mtu sahihi, Lakini haikuwa hivyo.

Changamoto zikawa nyingi, Ghafla hakuwa Coutinho yule tuliyemfahamu akawa Coutinho wa kutolewa kwa mkopo na majeraha yakiwa kando yake. Kwa sasa yupo QATAR nani anajali? 

Coutinho wa Liverpool alikuwa mchezaji hatari zaidi, Kwenye kiungo mshambuliaji alifanya kazi kubwa sana, EPL haiwezi kumsahau Coutinho kirahisi.

Sina uhakika sana lakini Labda kuna muda Coutinho anatamani siku zingerudi nyuma kama Linex Ili alekebishe alipokosea, Labda aliondoka Liverpool mapema.

 Wakati namsikiliza Linex, Nikapata muda wa kumkumbuka yule fundi wa Brazil, Phillipe Coutinho wa Liverpool.

Alitamba sana akiwa Anfield na jezi yake namba kumi mgongoni na hakuna timu ambayo barani Ulaya isingependa kuwa naye kwa kipindi kile.

Philipe alifanya kila kitu kwenye mpira na mpira ukamtii kama ambavyo mwanamke ana mtii mume wake kwenye ndoa.

Kwa bahati mbaya tamaa ziliweza kumfanya aondoke Liverpool na kujiunga na Barcelona na baada ya kufika Hispania taiifa Ambalo ni ndoto za wachezaji wengi duniani mambo yalienda kwenda tofauti na vile ambavyo alitarajia.

Philipe alianza kukaa sana benchi pale Barcelona mpaka baadae ikabidi atolewe kwa Mkopo kwenda Bayern Munich ili aweze kurudi lakini kwa bahati mbaya mambo yalienda tofauti na matarajio ya wengi.

Bado aliendelea kuandamwa na mashetani ya Anfield na hata ile mizimu ya the baviariani haikuweza kusikiliza kilio chake hata kidogo.

Baada ya kutembea kwenye hizo timu zote na kushindwa kuonyesha uwezo mkubwa akajiunga na Aston villa ya Unai Emiry kwa bahati sana hajafanikiwa pia kufanya vizuri ikabidi atolewe kwa mkopo kwenda Al duhail na bado mambo ni magumu

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement