Mashabiki 75000 walikuwa wanaimba kwa shangwe sana. Hatuna shule hatuna meya wa jiji, hatuna maji safi, hatuna ajira, hatuna mabasi haya yote kwetu hayana maana kwa sababu tuna Maradona.

 Alisema hana uwezo wa kuwalipa bali kuwafurahisha uwanjani.

 Wakati Papa Julius wa pili anafungua makumbusho ya Vatican mwaka 1506 alichukuliwa kama kiongozi mkatili asiyeogopa. 

wengi walishangazwa na uamuzi wake lakini mpaka leo zaidi ya watu million moja wametembelea pale. 

Ni makumbusho pekee kuna jezi ya Maradona iliyosainiwa na Papa Francis. 

Waumini wengi walishangazwa na maamuzi ya Papa Francis kuitunza jezi ya Maradona wengi waliamini ni mhuni . 

Wakati River plate wanahitaji huduma yake alichagua Bocca Junior timu ya nyumbani na mtaani kwao pamoja ya kudumu mwaka mmoja pekee. 

Akiwa na miaka 23 alikuwa mchezaji wa kwanza kutokea Barcelona aliyepewa gwalide la heshima na mashabiki wa Real Madrid kwenye mechi ya El Classico mwaka 1983 . 

Pamoja na kipaji chake kikubwa zaidi ya mashabiki laki mbili walishinikiza aondoke Barcelona.

 Kando ya bahari ya Mediteranea watu zaidi ya million tatu Maradona alikuwa anatambuliswa kwenye timu ya Napoli uwanja wa Stadio San Paolo kipindi hicho mnamo July 5 mwaka 1984.

 Mwandishi nguli David Goldblatt alitamka maneno mazuri alikuwa anasema mkombozi amekuja mashabiki kwa furaha walikuwa wanaitikia Diego Maradona. 

Walishinda ubingwa wa kwanza na jiji la Naples walifanya sherehe kwa wiki nzima. 

Magazeti nchini Italia yalipamba jina la Maradona Ufalme mpya umezaliwa. 

Watoto waliitwa jina lake ili kumuenzi. Majengo ya Naples yalipambwa picha za Maradona. 

2002 Fifa walipotangaza goli lake mbele ya England kuwa bora kwenye michuano ya kombe la dunia yeye aliamini goli la mkono wa Mungu lilikuwa bora.Jezi yake ilitunzwa na mwaka huu imepigwa mnada zaidi ya Billion 10. 

Waandishi nguli Rogers Bennett na Kelvin Baxter walisema ni moja ya wachezaji bora kuwahi kutokea waliofanya vizuri kwenye michuano ya kombe la Dunia.

Waandishi nguli Rogers Bennett na Kelvin Baxter walisema ni moja ya wachezaji bora waliowahi kufanya vizuri kwenye michuano ya kombe la Dunia.

 Pamoja na kuhusika kwenye matukio ya matumizi ya madawa kama cocaine pia alihusika katika matukio mengi ya kijamii. 

Aliwahi kucheza mechi nyingi ili kusaidia taasisi za kijamii aliokoa maisha ya watoto wengi sana.

 Alizunguka nchi nyingi na viwanja vingi kucheza mechi za hisani akiwa na marafiki zake Pele, Platin na Ronaldo. 

Walimuita ELI PIBE DE ORO kwa maana ya malaika mwenye sura chafu.

Kuna wachezaji ni bora kuna wachezaji wameacha alama kubwa kwenye hii Dunia ni ngumu hata kuwaandika ila nimechagua jina la Maradona.

Kwangu mimi ni moja ya wachezaji bora nimepata nafasi ya kuandika chochote. 

Argentina wana Messi ila bado wanapata ukakasi sana kusahau Jina na ubora wake. Ametwaa Taji la Kombe la Dunia na imekuwa ndoto ngumu kwa Messi .

Anaenda kujaribu bahati yake ya mwisho Qatar sijui atashinda ila bado Maradona anabaki bora. 

“Ni habari ngumu na za kusikitisha sana. Nimempoteza rafiki mkubwa ila Dunia imempoteza Gwiji.

 Kuna mengi ya kuzungumza ila kwa sasa namuomba Mungu aipe nguvu familia kwenye hiki kipindi kigumu Siku moja nina matumaini tutacheza tena mbinguni” yalikuwa maneno ya Pele. Ilikuwa November 25, 2020.

 Familia ilitangaza kifo chake Dunia ilikuwa inaomboleza, wachezaji wengi waliguswa na kifo chake mashirikisho mengi duniani yaliguswa na kifo chake.

Tanzania kupitia Azam Tv walisimamisha dakika moja kuomboleza kifo chake kwenye mechi ya Azam na Yanga.

Mbele kabisa kwenye kurasa za wachezaji bora kuwahi kutokea sijui nani ataanza ila namba mbili nitaandika jina la Diego Maradona. 

Alibadilisha maisha ya Napoli walimuona kama Mungu mpaka leo uwanja wao unaitwa Diego Armando Maradona stadium.

 “Hata kama nikicheza kwa miaka million moja siwezi nikafikia ubora wa Maradona sio kwamba sitamani kufikia mafanikio yake ila ni mchezaji bora kuwahi kutokea” Yalikuwa maneno ya Lionel Messi. 

Huenda nisipate tena nafasi ya kuandika ila angalau nimeandika chochote kuhusu Maradona. Que descanse en paz Maradona.



Imeandaliwa na: Fatuma Rashid.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement