Naiona Bato tamu ya Vigogo Vijana ndani ya Dimba la Mkapa na Loftus Versfeld kule Pretoria nchini Afrika Kusini.

Ni Bato Tamu ambalo naamini litakuwa na ushindani wa aina mbili, kwanza ndani ya Uwanja na nje ya Uwanja.

Ndani ya Uwanja nikimaanisha vikosi vyote viwili, Dar sa salaam Young Africans na Masandawana “Mamelodi Sundowns” huku nje ya Uwanja nikimaanisha kwa vigogo wawili vijana wanaoziongoza Klabu hizo.

Yanga ambao ndio wenyeji katika mchezo wa kwanza na watakuwa wageni Aprili 05 kule Afrika Kusini kwenye Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika iko chini ya Rais Hersi Said ambaye ndiye mtu aliyesimama nyuma ya mafanikio ya mabingwa hao wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara kwa kipindi cha miaka mitatu.

Hakuna mchezaji aliyepo ndani ya kikosi hicho hajapitia kwenye mikono ya Hersi kuanzia usajili mpaka sasa alipo ndani ya timu hiyo.

Maisha hayohayo amekuwa nayo pia Tlhopie Motsepe, mwenyekiti wa Mamelodi Sundowns akichukua kiti hicho kutoka kwa Baba yake Dk Patrice Motsepe ambaye aliona Klabu hiyo itakuwa kwenye mikono salama mbele ya kijana wake huyo wa kiume aliyekuwa karibu naye wakati akiwa klabuni hapo.

Hersi na Fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika huku Tlhopie akiwa ni Bingwa wa African Football League “AFL”  

Hersi ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Klabu za Afrika rekodi kubwa ambayo anatamba nayo ni kuifikisha Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na klabu ya Yanga ambayo ilicheza kwa mara ya kwanza msimu uliopita ikiwa ni rekodi kubwa ya Klabu hiyo.

Upande wa pili, Tlhopie amefanikiwa kuweka kabatini Ubingwa wa Afrika Football League ikiwa ni Klabu ya kwanza kuchukua Ubingwa huo wa mashindano hayo makubwa ya Klabu yaliyoanza mwaka jana.

Kunakitu kinaitwa Convincing Power, Hersi na Tlhopie kila mmoja akiwa na Klabu yake, wamekuwa wakijitambulisha kwa kuishi karibu na wachezaji wa timu zao, Kila mmoja amekuwa na nguvu yake katika ushawishi wa kutafuta matokeo na hata rekodi mbalimbali za Klabu zao hizo mbili jambo ambalo limewajengea Imani kubwa na wachezaji kuzipigania klabu hizo Uwanjani.

Ninamuona Eng: Hersi na GSM huku Tlhopie na Motsepe, Huwezi kumtofautisha Hersi na Ghalib Said Mohammed ambaye amekuwa mfanikishaji wa karibu kila kitu kuhusu jeuri ya Yanga kifedha kuanzia usajili mpaka maisha mengine ya gharama kubwa.

Ni hivyo hivyo kwa Tlhopie naye amekuwa na nguvu kubwa ndani ya Klabu yao kutokana na nguvu ya kifedha ya baba yake ambaye ni tajiri mkubwa wa biashara ya madini nchini Afrika Kusini.

Mamelodi Sundowns imekuwa na nguvu ya kusajili mastaa ghali kutoka nje ya Afrika kutokana na ukwasi wa Motsepe ambaye yumo kwenye orodha ya matajiri 10 bora barani Afrika.

Hersi na Tlhopie wote ni vijana, kila mmoja amekuwa maarufu eneo lake kutokana na mwonekano wa mawazi yao.

Ilizoeleka watu wa nafasi zao huku nyuma kuwaona wanavaa mavazi ya suti kila wakati. Lakini kwa vijana hawa wawili ni toauti.

Wakati Hersi anaingia madarakani ilikuwa ikielezwa viongozi wanaovaa suruali aina ya jeans zilizotoboka itakuwa vigumu kuipa klabu hiyo matokeo, lakini mpaka sasa amekuwa akijitambulisha kwa mafanikio bila kuwa na anguko.

Kama ilivyo kwa Tlhopie, kwani ukimkuta katika maeneo yake ya kujidai unaweza kubisha kwamba si mwenyekiti wa Klabu hiyo, kwa umri alionao na hata mavazi yake ya ujana.

Wote wakiwa Nadhifu mwilini na Smati zaidi kichwani.

Jumamosi na Aprili 05 wote watakuwa kwenye Jukwaa kuu Viwanjani wakiziongoza Klabu zao kupambana kwa mara ya pili katika historia ya timu hizo, lakini safari hii zikiwa na viongozi vijana.

Acha tukaione vita ya kibabe.

Mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana ilikuwa katika mechi za raundi ya pili ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2001, ambapo mamelodi alishinda bao 3-2 nyumbani kisha kupata sare ya bao 3-3 ugenini ambapo Yanga aliaga michuano kwa Jumla ya mabao 6-5.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement