Jude Bellingham

alikuwa na mafanikio makubwa huko Dortmund, baada ya kuchukuliwa kutoka Birmingham City mwaka wa 2020 kwa ada ambayo ilimfanya kuwa kijana ghali zaidi wa miaka 17 katika historia. Pesa hizo zilionekana kutumiwa vyema na BVB huku Bellingham akiingia kwenye kikosi cha kwanza haraka na baadaye kuwa mchezaji muhimu, akiichezea klabu hiyo mechi 132.

Haraka sana, alikuwa akihusishwa na baadhi ya klabu kubwa za Ulaya. Mnamo 2022, alikataa kuhama lakini miezi 12 baadaye, Liverpool na Manchester United timu hizo zinazompigania, alichagua kuhamia Real Madrid.

Ousmane Dembele

Baada ya mabao 10 na pasi 21 za mabao katika mwaka wake wa kwanza huko Dortmund, Barcelona walipata pesa ya kumnunua Mfaransa huyo kufuatia kumpoteza Neymar ambaye amenunuliwa na Paris Saint-Germain msimu uliopita wa joto 2017.

Dembele alifanikiwa Kuifungia klabu ya Dortmund mabao 72 Bundesliga.

Hata hivyo, tangu ajiunge na Barcelona, ​​Dembele amekuwa na matatizo ya majeraha na hafanani kabisa na Dortmund yake.

Jadon Sancho

aliwasili Borussia Dortmund akiwa jamaa asiyejulikana kutoka akademi ya Manchester City, aliacha kampeni ya ushindi wa Kombe la Dunia la U17 mapema na kujiunga na kikosi cha Dortmund mwanzoni mwa msimu.

Baada ya muda mfupi wa kuzoea huko Ujerumani, Sancho alianza kuandika vichwa vya habari kwa maonyesho yake. Alikuwa kiongozi wa wachezaji wachanga wa Uingereza waliohamia nje ya nchi na alichangia zaidi ya mabao 100 katika mechi 137 pekee za klabu kabla ya kurejea Ligi Kuu.

Christian Pulisic

alikuwa na umri wa miaka 20 tu wakati Chelsea ilipomtambua kama mbadala wao wa Eden Hazard. Pulisic ambaye ni mchezaji wa kuchezea chenga, alishindana na Sancho kwa ajili ya mechi ya kuanzia wakati wa ujana wao kwenye klabu hiyo na Mmarekani huyo alifanikiwa kuhamia moja ya vilabu vikubwa zaidi barani Ulaya mnamo 2019.

Pierre-Emerick Aubameyang

alishindana na Robert Lewandowski kuwania taji la mshambuliaji bora wa Ujerumani wakati alipokuwa Dortmund.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Gabon alifaa kabisa kwa mtindo wa kasi wa juu wa BVB, wa kushambulia na Alishinda Kiatu cha Dhahabu cha ligi msimu wa 2016/17, akifunga mabao 31 katika michezo 32 pekee ya ligi. Aliondoka klabuni hapo akiwa na bao 93 na mataji matatu.

Erling Haaland

amekuwa mchezaji kwa mauzo katika historia ya Dortmund baada ya kuhamia Man City. Raia huyo wa Norway amefanya vyema nchini Ujerumani na alianza maisha yake ya Dortmund kwa mtindo mzuri kabisa, akifunga hat-trick akitokea benchi kwenye mechi yake ya kwanza. Kwa jumla, Haaland alifunga mabao 85 katika mechi 88 pekee za Dortmund tangu ajiunge nayo kutoka RB Salzburg na kutoa pasi za mabao 23. Kipaji cha supastaa, mara moja alionyesha kipaji chake akiwa na Manchester City, akiweka rekodi ya kufunga mabao kwenye Ligi Kuu ya Uingereza katika msimu wake wa kwanza.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement