Watoto wa Kiingereza wangesema "He's a legend in my Book " , Watoto wa Kiswahili wangesema "Ni Gwiji kwenye Kitabu changu .

SITTING BULL, Kiongozi wa jamii ya Hunkpa Lakota kabla hajafunga macho na kuonja Umauti aliwahi kunukuliwa akisema " if we must Die ,We die defending our rights " .Yeees kama Ni kufa inabidi tufe tukizilinda haki zetu .

Arsene Wenger ,Msingi wa Mpira wenye kuvutia kwa Arsenal aliwahi kunukuliwa akisema " Football is an Art ,Like Dancing is an Art , but only when it's well done does it become an Art" . 


Leo Kwenye kumbukumbu zangu nimeikumbuka Atletico Madrid ya Diego Simmione, leo nimeikumbuka Atletico Madrid ile ya Moto sana huku Barca na Real Madrid wakiwa na vipaji kama MSN na BBC .

Ni Atletico Madrid iliyojaa wengi wenye vipaji kama Gabriel Luis "Gabi",Juan Francisco "Juanfran",Tiago Cardoso Mendes na vizazi vya Mbeleni kama Antonie Griezman.

Muda hausimami na Mungu hutoa nafasi moja pekee ,anaweza akatoa nafasi ya kujifunza na kufurahia kitu fulani alafu asirudie tena kukupa hiyo furaha kupitia hicho kitu . Burudani ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ipo mwishoni,tulileta Ubishi juu yao ,hatimae muda umeisha .

Kwenye Atletico Madrid bora sana basi kwenye ukuta wao alikuwepo Kiongozi , hakuvaa usinga kama GABI. Ijapokuwa alikuwa Kiongozi mwenye heshima kiwanjani kisa Ukatili wake .

Kwa Majina aliitwa Diego Roberto Godín Leal.Kiufupi ni DIEGO GODIN , Jezi namba 2 Mgongoni kwenye Uzi wa Atletico Madrid na Jezi nambari 3 kwenye Uzi wa Uruguay.


Sio bora wa muda wote kama Fabio Cannavaro na Paolo Maldini kwenye Soka ,Lakini kwa Kizazi hichi cha watu kama Sergio Ramos, Chiellini, Bonnuci ,Pepe na wengineo basi na yeye ni bora.

Diego Godín ameacha alama kwenye Soka , ameshinda vingi akiwa kwenye Timu yenye Ukawaida hadi ikawa tishio . Kuingia kwenye Kikosi cha UEFA CHAMPIONS LEAGUE kwa mara tatu sio kitu kidogo ni ubora ambao ulikuwa ukiongea kutoka Kwa Mzawa wa Rosario del Colla, Uruguay. 

Hadithi ya mtu huyu taanza kuitoa kwa Wajukuu zangu ,tawapa Hadithi ya mtu chuma ambaye waingereza wangemuita "UNDERRATED " Kama Stamina wa Moro alivyojiita .

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement