Juni 22 mwaka 2022 mchezaji nyota wa kike kutoka Tanzania, Clara Luvanga aliposti picha kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram akiwa anatazama kitu kupitia darubini ndogo ya mkononi na kuandika maneno yaliyoonyesha ni kwa namna gani anamkubali Supastaa wa Kireno, Cristiano Ronaldo ambaye ni mshindi wa Ballon d’Or ya mwakasoka bora wa Dunia.

Wakati Luvanga anaweka Posti hiyo, Ronaldo alikuwa amerejea nyumbani Manchester United akitokea Real madrid huku Luvanga alikuwa zake Tanzania na hakuwa hata akijua kama ipo siku atakuja kucheza klabu moja na supastaa huyo pamoja na kwamba yeye anacheza soka la Wanawake na CR7 kwa upande wa Soka la Wanaume.

Clara alijiona kama CR7 vile na ndio maana hata vifupisho vya majina yake vya CL akavibadili kidogo na kuandika CR ili kufanana na vya mchezaji huyo ambaye alionyesha wazi kuvutiwa naye.

Nani anaijua kesho yake? Waswahili hupeda kusema kuwa ni Fumbo kuijua kesho yako, licha ya changamoto nyingi alizokuwa akikumbana nazo aliweza kuruka viunzi hivyo na hatimaye kuonyesha kuwa anatamaa ya kufikia mafanikio.

Ndoto zake hazikuwa Tanzania, alipata shavu la kwenda Hispania, timu ya Ligi Daraja la pili, Dux Logrono na wakati huo Ronaldo alikuwa ametimiza miezi nane ya kucheza soka la kulipwa Saudia baada ya kufanya uamuzi mgumu wa kuondoka Manchester United kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na Kocha wa Timu hiyo, Erik Ten Hag ambaye alikuwa akimsugulisha Benchi.

Licha ya kuwa nje kwa kipindi kirefu, Clara alianz ana moto wake huko Hispania kiasi cha kucheza kwa kipindi kifupi mno na ndipo Al Nassr ya wanawake ambayo ilikuwa katika kukijenga kikosi chake ilipovutiwa na mshambuliaji huyo na kuamua kumsajili.

Kitendo cha Clara kutokea Hispania ambako Ligi kuu ilikuwa ikiendelea, kilimfanya kuwa moto wa kuotea mbali na moja kwa moja aliingia kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya Wanawake ya Al Nassr na kugeuka kuwa Tunu kwao.

Huku Ronaldo alikuwa akikiwasha kwa upande wa wanaume, akifunga mabao kila uchao na kwa upande wa pili kwenye Ligi ya wanawake Clara naye alikuwa akijibu mapigo kwa kuwapa raha mashabiki wa Al Nassr.

Nyota hao walijikuta kila mmoja anakuwa kinara wa mabao kwa upande wake.

Clara ameimaliza kazi yake ya kuisaidia Klabu yake ya Al Nassr kutwaa Ubingwa wa Ligi kuu kwa Wanawake, vita iliyosalia mbele yake ni kwenye ufungaji bora ambapo anaongoza akiwa na mabao 11 huku ikisalia michezo miwili.

Kwa upande wa wanaume, Ronaldo anaonekana kuwa bado na kibarua cha kufanya kutokana na utofauti mkubwa wa pointi 12 uliopo baina ya Al Nassr wenye Pinti 56 na Al Hilal wenye Pointi 68 ambao wanaongoza msimamo wa Ligi hiyo.

Kwa upande wa kuzifumania nyavu, Ronaldo anaongoza akiwa na mabao 23, amemzidi Aleksandar Mitrovic wa Al Hilal.

Siku zote tunatakiwa kutokukata tamaa, Uvumilivu wa Clara unaanza kumlipa

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement