Kwenye mechi 29 za NBC Premier League Azam Fc imefunga magoli 61, magoli 6 nyuma ya Yanga Sc iliyofunga magoli mengi zaidi msimu huu.

Sio kitu rahisi hususani duru la raundi ya pili mechi nyingi wamecheza bila kuwa na mshambuliaji HALISI (namba 9).

Hapa sasa ndio ninaporudi kwenye eneo la benchi la UFUNDI la Azam Fc (Bruno Ferry na Yousuf Dabo) wawili hawa kuna kitu kikubwa wamekitengenza kwenye kiwanja cha mazoezi(Programs) na wachezaji wake wakakipokea vizuri na kutimiza majukumu vyema ndani ya kiwanja.

Mbinu na ubora wa vichwa vya makocha hawa wawili Kwa pamoja ndio wamefanya tuone Azam Fc ikiwa bora sana kwenye eneo la tatu ya mwisho (Final third)

Dube hayupo kikosi, Allasane Diao ni majeruhi (ila kukosekana kwao hakujaathiri system ya uchezaji na muundo wa timu).

Azam Fc Wana utajiri wa viungo washambuliaji wengi wenye uwezo mkubwa kiufundi, uwezo wa kufunga magoli na kupika magoli.

Kipre Jr,Sopu kuna nyakati tofauti tofauti wanatumika kama FALSE 9,na bila ajizi wanapiga Kazi vizuri wakati nyuma yupo Fei Toto kama NAMBA 10.

Lakini ni Dabo HUYU huyu anayefanya mabadiliko na kumuona nyakati nyingine Kipre Jr akicheza kama INVERTED WINGER

Kushoto Kipre Jr,kulia Sillah(bomu hili) halafu benchi kuna wachezaji kama Iddy Nado na Ayoub Lyanga, Dabo hizi ndio silaha zake za maangamizi na so far zimemlipa vyema kabisa.

Ili timu ya mpira iwe imara LAZIMA vitu vya msingi kwa kila upande viende sambamba.

Akili ya ubongo ya mwalimu ndio itapelekea afanye machaguzi sahihi ya mchezo kulingana na mpinzani, halafu ustadi wa kiufundi (technical proficiency) ya wachezaji ndio italeta matokeo chanya.

Kitaalam: Mental intelligence+tactical approach+technical proficiency= Good results. 

Hapa ndio mpira wa miguu unapojitofautisha na siasa, kwasababu ni mchezo wa wazi kocha akifeli kichwani (kimbinu) basi ndani ya kiwanja atapoteza mchezo.

Naiona Azam Fc tishio kwenye msimu ujao,na hii ni kwasababu Dabo tayari ametuonesha sura yake ya kimbinu, zakazakazi miaka miwili mbeleni naona ubingwa ukija Chamazi.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement