Katika kipindi nilichoanza kuujua/kufuatilia mpira wa miguu sijaona kiungo aliyekua na usahihi wa kupiga pasi ndefu nyingi na kufika kwa usahihi zaidi ya CHUJI.

CHUJI kiraka wa mpira 4 alibonda hapo shilingi 6 ndio uwanja wake wa nyumbani kuna nyakati fulani aliwahi kutimika kama kiungo wa pembeni HALF SPACE MIDFIELDER kwenye timu ya taifa (Taifa Stars) na alifanya vyema sana.

Nimeshuhudia viungo wengi kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 2000 mpaka leo hii.

Mamido kama Waziri Mahadhi, Salvatory Edward Augustine, Seleman Matola, Christopher Alex,Shabani Kisiga, Yusuf Rwende Macho Musso, Shekhani Rashid, Abdulhareem Humuod,Juma Sefu Kijiko, Mwinyi Kazimoto, Nico Nyagawa, Geoffrey Bony Ndanje, Jonas Mkude na wengine wengi ila CHUJI anabaki kuwa alama ya kiungo mwenye uwezo mkubwa wa kupiga Pasi ndefu kwa usahihi.

Switching play zake one of the best kwenye pasi hizo.

Hapo angalau marehemu Geoffrey Bony Ndanje, Matola ndio pengine wanafuata kwenye upigaji wa pasi ndefu.

Chuji katika ubora wake alikua sio poa, alifanya mabalaa mengi shimoni + kufunga magoli.

Nyakati zinakimbia,watu wanapotea wengine wanaibukia lakini mpaka sasa sioni master wa hizi pasi hata kwa wachezaji wa kigeni.

Legend nimekumbuka enzi zako faza.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement