MWAKA 2015, wakati akizungumza na chombo cha habari cha British Broadcasting, maarufu kama BBC moja wa makocha wa zamani wa Anthony Martial, bwana Aziz Benaaddane alikuwa akimueleezea Martial kwa ufupi.

Aziz alikuwa kocha wa Martial katika timu ya Les Ulis wakati Martial akiwa kijana mdogo, alisema kuwa walipata vijana 400 wenye uwezo wa mpira ila hawakuwahi kuona kijana mwenye uwezo wa ajabu kama wa Martial. 

Alisema kuwa kuwapata watu mithili ya Martial unaweza kusubiri baada ya miaka mitano au sita kuwapata kwa kipindi kile, hivyo waliamua kuendelea kumuongezea baadhi ya vitu Martial aendelee kuwa bora zaidi.


Mahmadou Niakite alikuwa ni kocha mwingine wa Martial alisema kuwa Martial japo alikuwa ana miaka 6 tu lakini alikuwa na uwezo mkubwa wa kucheza kwenye makundi mengine yenye umri mkubwa zaidi yake.

Huko kote ni safari za Anthony Martial, kijana ambaye ana kipaji cha ajabu, kipaji kilichomfanya mwandishi wa habari, Phillipe Auclair kusema anacheza kama mzee wa kutembea kwenye chaki, Thierry Henry.

Tarehe 1 Septemba 2015, Louis van Gaal akamwaga kiasi cha pauni milioni 36 pale AS Monaco, Martial akaja Uingereza kwenye jiji la Manchester, tukamjua, kwa sababu wengi hatukumjua sana.

Tarehe 12, Septemba, Juan Mata anatoka nje dakika ya 65, jezi na 9 mgongoni Anthony Martial anaingia uwanjani, ninachokumbuka ni kile alichowafanya wale waliverpool Martin Skrtel na Dejan Lovren, anapigilia msumari wa 3, Liverpool anakufa 3-1 Old Trafford. The New boy has arrived in town! Unacheza na waingereza nini?

Katika michezo minne ya awali akiwa na Mashetani wa Manchester akapiga kamba nne, akatulia kama sio yeye. Nani kama Van Gaal? Tukampa sifa zake.

Baada ya huo msimu kumalizika, Martial hajapotea, ila amekuja na tabia moja mbovu na ya kihuni sana japo kuna muda inakuwa na faida sana.

Kuna wakati wana Manchester wanataka mabao yake, hasa yale ya wazi anayoyakosa kipindi bado kuna dakika nyingi, lakini kwa wakati huo yeye ni kama shetani mwovu kwa wakati huo, hawapi kile wanachokihitaji.

Ni kweli watamuita mvivu, watamwambia Ole ampeleke benchi lakini hayo yakitokea, utamuona Martial amesimama kwenye kibendera, ameshafunga goli, mashabiki wanashangilia Mike Dean au Martin Atkinson ameitisha ngoma kati, hapo amekuwa malaika mwema katika wakati ambao mashabiki wameshamkataa.


Ameshapiga zaidi ya mabao 10 msimu huu, wakati mkimuhitaji yeye hataki kuja, wakati mnasema hafai, yeye anawafanya mambo ambayo yanadhihirisha anafaa, kwa sababu mabao yake ni ya muhimu sana.

Sio tabia nzuri, ila naona amempata rafiki mzuri anayempenda, anayetaka afunge kila muda. Anaitwa Bruno Fernandez, Bruno hapendi uvivu, najua hapa Martial hata asipotaka atakuwa muhimu kwa muda wote.

Kwa bahati mbaya amekuja Bruno lakin ule mwanga wa matumaini ya kuliona jua umepotea , hakuna matarajio ya ujio mpya wa Antony Matial kwenye kikosi cha Manchester united licha ya kuja nyota wengi wenye ubora wa hali ya juu .

Matumaini yalikuwa kwa Sevilla baada ya kupelekwa pale kwa mkopo mwaka 2022 lakini kwa bahati mbaya mambo hayajawa mazuri na mpaka hivi sasa yupo Manchester united lakini haijulikani atarudi lini kwenye ubora wake ikiwa ni miaka 28 sasa

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement