AKILI NA HEKIMA YA DR. MSHINDO MSOLA ILIVYORUDISHA MATAJI YANGA AFRICA
Ni iyena Iyena na shangwe zimetawala kila kona ya mitaa, kuanzia mitaa ya Twigwa na jangwani,Ubungo mataa na kimara Temboni,Usijiulize kunani ni Yanga bingwa jamanii..!! ,Tena uliochagizwa na Pointi 6 Za mtani,kwa kipigo cha nje ndani.
Kweli nyakati ngumu hazidumu,na siku zote wakati ndio hutoa hukumu, bando najiuliza hivi hawa ndio wale walioakuwa wanaendesha timu kwa kutegemea bakuli,waweze kushindana na Jirani mwenye misuli,Aisee kweli wametoka mbali lakini sio kwa kumfuata Miso misondo ila kwa Kufuata dira ya Mshindo Msola,
Mzee mwenye maarifa ya kutosha na hekima aliyejipa Kazi ngumu Ya kuitoa Yanga Africa kwenye Udhaifu na Unyonge Hadii kwenye Nchi Ya Uzima,kuwavusha kwenye kumtegemea Ditram Nchimbi,Sapong Na Juma Balinya Hadii kufikia kwenye Zama za Mayele Mzee wa Kutetema hadii nyakati hizi za sasa za Guede Kafunga Tenaa.
Akili Yake ndo Ilimshawishi Kabaila Gharibu Said Mwana Wa Ruvuma, Kufungua Pochi kuboresha kikosi na Kuwaunganisha wananchi kuwa kitu kimoja Ili kuleta utulivu na Ukimya.
Hekima yake ilimfanya kukubali Kuiacha Timu kwa hao tunaowaimba wanaijenga Yanga licha Ya kubezwa kuwa bado ni Vijana yaani Arafat na Hersi kipenzi cha mashabiki na wanachama.
Nimemkumbuka Daktari huyu wafalsafa kitaaluma ambae aliamini Panahitajika Mabadiliko ya Uendeshaji ila kwa kutegemea Nguvu ya wanachama,Ili Timu iweze kijiendesha kwa kujitegemea Ili wasirudi kwenye nyakati za nyuma.
Akili na hekima yake imewarudishia Heshima Back to Back ya Makombe na hizo iyena Iyena na shangwe ni kwa mara ya tatu Tena,huko Afrika Sasa ni washindani sio washiriki Tena.
Nafsi yangu inaamini Ni yeye ndio chanzo cha haya yote,Na kwangu hatabaki kuwa kiongozi bora wa Yanga Afrika kwa nyakati zote,kwa sababu ndio aliyejenga misingi ya Yanga Afrika kuwa Timu ya watu wote.