Bouchra Karboubi ni msimamizi wa sheria. Akiwa uwanjani anatumia filimbi na kadi zake kuimarisha utulivu lakini katika kazi yake ya kila siku, pingu ndilo linalomsaidia.

Karboubi ni mwamuzi wa kimataifa wa mpira wa miguu na polisi mwanamke huko Meknes, jiji la kaskazini mwa Morocco.

"Kuwa polisi mwanamke kwangu, kunamaanisha kutumia haki,"

"Kama mwamuzi, mimi hutumia sheria na ni kazi na ni kazi yangu ninayoipenda na zote mbili zina uhusiano."

Karboubi ndiye muamuzi pekee kati ya maofisa sita wa kike wa mechi katika Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 nchini Ivory Coast.

Mnamo 2022, Salima Mukansanga wa Rwanda aliandika historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuwa muamuzi wa mechi ya Afcon ya wanaume nchini Cameroon.

Karboubi aliiga hilo mwezi uliopita, na aliongoza timu ya maafisa wa timu ya wanawake - mchuano mwingine wa kwanza - wakati Nigeria ilipoishinda Guinea-Bissau katika hatua ya makundi.

Jukumu kuu la alilonalo Mmorocco huyu katika michuano inayoendelea linamfanya kuwa mwanamke wa kwanza kutoka Afrika Kaskazini kuwa muamuzi katika Afcon ya wanaume.

"Hisia zilikuwa kubwa sana. Ni heshima kwangu, kwa familia yangu, kwa nchi yangu na kwa wanawake wa Kiafrika kwa ujumla," anasema kuhusu ushiriki wake.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 36, hata hivyo, anaongeza kuwa kuna zaidi ya utambulisho wake zaidi ya kazi zake mbili.

"Ni kweli kazini mimi ni askari polisi na uwanjani ni muamuzi, lakini nyumbani mimi ni mwanamke, mimi ni mama wa nyumbani na mama wa binti."

Katika ukuaji wake, Karboubi alipenda kucheza soka lakini aliacha kwa sababu hakukuwa na soka la wanawake lililopangwa wakati huo.

Kwa hivyo, aliamua kuingia kwenye mechi ambapo aliona fursa nyingi zaidi kama muamuzi.

Karboubi alikabiliwa na upinzani kutoka kwa familia yake katika kufuata ndoto zake, akiwaambia Wanawake wa Muungano wa Mataifa wa Kiarabu, ya nje mnamo 2021: "Ninatoka katika mji mdogo wa kihafidhina; kwa hivyo, ilikuwa ngumu kwa familia yangu kukubali ukweli kwamba nilitaka kuendeleza taaluma yangu ya michezo."

Ndugu zake ndio walikuwa kikwazo chake kikubwa.

Waliwahi kupata bendera ya msaidizi wake na kuipasua na kumwacha kijana Karboubi akilia lakini aliishona na kuendelea na mazoezi.

Lakini mwaka wa 2007, baba yake alimtizama akiwa muamuzi wa mchezo wa wanawake, na kuanzia hapo alipata usaidizi wa kufuata njia aliyochagua. Leo, yeye ni muamuzi wa kwanza mwanamke wa Kiarabu uwanjani.

Kando na kuwa mwanamke wa kwanza Mwarabu kuwa mwamuzi wa mechi ya wanaume mnamo 2020, Karboubi pia ndiye mwanamke wa kwanza Muafrika kufuzu kama mwamuzi msaidizi wa video (VAR).

Morocco na Misri ndizo nchi pekee barani Afrika ambazo zimetekeleza kikamilifu matumizi ya VAR katika ligi zao za ndani.

"Nina bahati kuwa Morocco kwa sababu ni nchi ilikuwa nchi ya kwanza ya Kiafrika kkuanzisha matumizi ya VAR," Karboubi anaelezea kuhusu jinsi alivyoanza kazi ya usimamizi wa video.

“Niliweza kuhudumu kama mwamuzi msaidizi wa video katika fainali ya Afcon ya 2021 kwa wanaume na ilikuwa heshima kwangu.

"Ilimaanisha kuwa wanawake wangeweza kufanya kazi katika maeneo yote kama wanaume. Daima tumepigana kuwa na wanaume. Tuliweza kuonyesha kwamba tunaweza kuwa [huko]."

Jukumu la kwanza la kimataifa alilotekeleza Karboubi kama muamuzi lilikuwa ni Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake 2018 nchini Ghana.

Waamuzi wa kike kote ulimwenguni wanafanya vyema kwenye mchezo huo mzuri.

Mnamo 2022, Stephane Frappart wa Ufaransa alikua mwanamke wa kwanza kuchezesha Kombe la Dunia la Fifa kwa wanaume, akisimamia mchezo wa hatua ya makundi kati ya Costa Rica na Ujerumani.

Licha ya hatua hizi zilizopigwa hadi sasa, Karboubi anahisi wanawake bado lazima wapige hatua ya ziada ili kuthibitisha umahiri wao.

"Ni kweli wanawake ili kufikia kiwango hiki lazima wafanye kazi ya ziada, kwanza kimwili, kwa sababu ili kuwa tayari kwa mechi ya wanaume lazima tuwe sawa sawa na wanaume," anafafanua.

"Baada ya hapo utaalamu wa kiufundi, ambao lazima tuwe nao bila shaka, juu ya sheria za mchezo.

"Mwanaume akikosea watasema yeye ni mwanaume, ni binadamu tu. Lakini mwanamke atakosolewa mara mbili zaidi kwa sababu ni muamuzi wa kike."

Akiwa kazini huko Morocco katika polisi, Karboubi ni Inspekta na hupata usaidizi kutoka kwa wafanyakazi wenzake ambao daima wana hamu ya kujua kuhusu majukumu yake ya oungozaji wake wa kazi

"Wananiambia maneno kama; 'Kwa nini haukufanya hivyo? Kwa nini ulifanya hivyo? Kwa nini ulipiga filimbi kwa penalti? Tueleze kwa nini kadi nyekundu' lakini daima wananitia moyo, na ninashukuru msaada yangu," Karboubi alisema.

Anaamini kwamba kazi hizo mbili zinafanana.

"Usimamizi ulinisaidia sana kama mwanariadha kuwa afisa mzuri wa polisi, na kuwa afisa wa polisi kulinisaidia kuwa mkakamavu uwanjani kama mwamuzi."

Akiwa ni mama wa mtoto mmoja ana matamanio ya kuchezesha Kombe la Dunia la wanaume siku moja, baada ya kusimamia kwa mara ya kwanza Fifa katika mashindano ya wanawake mwaka jana.

Anatumai kuwa mafanikio yake hadi sasa katika nyanja mbili zinazotawaliwa na wanaume yanaweza kuwatia moyo wanawake vijana katika ulimwengu wa Kiarabu.

“Inawezekana ilikuwa ni fani iliyotawaliwa na wanaume, lakini leo tumeweza kuonyesha kwamba hata wanawake wanaweza kufanya hivyo,” alisema.

"Kwa hiyo, ningewaambia wasichana ambao wana lengo hilo kufanya kazi kwa bidii na kamwe wasikate tamaa."

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement