ZIARA MAALUM YA MPIRA MKUBWA WA BASEBALL IMEVUNJA REKODI YA DUNIA YA GUINNESS
Ziara ya mpira huo wenye urefu wa futi nane (8) ilianza mnamo Juni 24 katika dimba la timu ya Indianapolis Indians (Victory Field) na kupita katika viwanja vingine 15 kabla ya kutua nanga jijini New York mapema wiki hii.
Wataalamu wa kukusanya takwimu za ‘Guinness World Records’ walithibitisha kuwa mpira huo unazo saini rasmi 6,750 na kuutaja mpira huo kuwa kifaa cha michezo chenye saini nyingi zaidi duniani.
Rekodi ya awali ilikuwa ikishikiliwa na klabu ya soka ya Cambridge United (England), ambapo wao walifanikiwa kukusanya saini 2,146 zilizowekwa katika jezi yenye ukubwa mara 40 ya jezi ya kawaida.



