Tanzania imekuwa miongozi mwa Mataifa 12 watakayowakilisha katika Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake , “WAFCON” 2024 Nchini Morocco mara baada ya Twiga Stars kufanikiwa kufuzu hapo jana mbele ya Togo kwa jumla ya ushindi wa bao 2-3.

Kocha wa Twiga Stars Bakari Shime, amekipongeza kikosi chake licha ya kupoteza katika mchezo huo wa marudiano kwa bao 2-0, ambapo katika mchezo wa awali Twiga Stars waliibuka na ushindi wa bao 3-0 mchezo uliochezwa Uwanja wa Chamazi Complex, Jijini dar es salaam.

“Dakika 90 zilikuwa dakika ambazo zinaushindani mkubwa, kwa ujumla mchezo ulikuwa mgumu sana kulingana na mechi yenyewe ilivyokuwa, tulikuwa na nafasi kubwa ya kushinda huu mchezo hasa kwa kipindi cha kwanza, tumetengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini kwa bahati mbaya washambuliaji wetu wamekosa umakini wa kuweza kuzitumia hizo nafasi, lakini yote kwa yote nawapongeza sana wachezaji wetu kwa kazi kubwa ambayo wameifanya wameliheshimisha taifa lao, ” Kocha wa Twiga Stars – Bakari Shime.

Kocha Shime ameongeza kuwa, licha ya kupoteza katika mchezo huo lakini wamejifunza vitu vingi na wanaamini vitawasaidia katika mashindano mengine yaliyo mbele yao.

Mbali na Tanzania, Mataifa mengine yaliyofuzu kushiriki Fainali za WAFCON 2024 Nchini Morocco ni Afrika Kusini, Botswana, DR Congo, Senegal, Algeria, Ghana, Tunisia, Zambia, Mali, Nigeria na mwenyeji Morocco.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement