Timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars jioni itashuka uwanjani kwenye mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya kuwania Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Wafcon) 2024 kwa kuvaana na Togo kwenye Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam.

Twiga inahitaji ushindi kwenye mchezo huo wa nyumbani ili kujitengenezea mazingira mazuri kwa mchezo wa marudiano utakaopigwa Desemba 5, ili kufuzu kwenda Morocco. Timu hiyo ilianza safari ya kwanza kwa kupokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Ivory Coast ugenini na kisha kumaliza kazi Azam Complex kwa ushindi wa mabao 2-0 na kuvuka kwa mikwaju ya penalti 4-2, wakati Togo ilianza kwa kuing'oa Djibouti kwa jumla ya mabao 13-0, ikishinda kipindi cha kwanza 7-0 na kisha 6-0.

Kiungo wa JKT Queens na Twiga, Donisia Minja alisema maandalizi yanaendelea vizuri na kama wachezaji wanatamani kufanya vizuri ili kufuzu michuano hiyo. "Ni muda mrefu hatujashiriki michuano hii, tutapambana kuhakikisha aliyotuelekeza Kocha wetu tunafanyia kazi" alisema Donisia, huku nyota wa kimataifa anayekipiga Eastern Flames ya Saudia, Enekia Kasongo baada ya kuwasili alisema; "Tunaamini kila mchezaji amejipanga vizuri kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Togo ili tufuzu hiko ndio kikubwa zaidi kwetu."

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement