Rais wa Shirikisho la Soka nchini “TFF” Wallace Karia ameweka wazi Imani yake juu ya Tanzania kufanya vizuri kunako mechi za kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika “AFCON2025” Nchini Morocco.

Rais Karia amezugumza hayo ikiwa ni muda mchache kabla ya kufanyika kwa droo hiyo Johannesburg nchini Afrika kusini ambapo Tanzania imeangukia Kundi H ikiwa na DR Congo, Guinea na Ethiopia.

Ni Nchi 48 za Kiafrika ambazo zinalenga kufuzu kwa toleo la 35 la onyesho la Afrika linalofanyika kila baada ya miaka miwili katika jaribio la kumuondoa kocha Emerse Fae wa Cote d'Ivoire kama wafalme wa bara akiwa ni Mwanaume aliyejizolea umaarufu kwa kuiokoa Cote d'Ivoire ikikaribia kuondolewa kwenye shindano lililopita - alikuwa miongoni mwa wasaidizi waliochaguliwa pamoja na gwiji wa Morocco Marouane Chamakh.

Cote d'Iovire wamepangwa Kundi G pamoja na mabingwa wa zamani Zambia, Sierra Leone, na Chad.

Misri, Taifa lililofanikiwa zaidi katika historia ya Kombe la Mataifa ya Afrika limepangwa katika Kundi ambalo wengi wanaamini ni gumu zaidi ambapo Mafarao hao ambao wameshinda AFCON mara saba, watacheza na timu mbili zilizo kwenye fomu, Cape Verde na Mauritania - Mataifa yote yalikuwa na matokeo ya kushangaza katika Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Cote d'Ivoire huku Botswana wanashika nafasi ya nne katika kundi C.

Wenyeji Morocco, wamepangwa katika Kundi B, watamenyana na Gabon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, na Lesotho. Simba wa Milima ya Atlas wakiwa na uhakika wa kushiriki kama wenyeji.

Mechi za kufuzu kwa Fainali hizo zitaanza Septemba 2024 na kukamilika Novemba mwaka huu wa 2024 huku Michuano hiyo ya Kombe la Mataifa ya Afrika ikipangwa kuanza kutimua vumbi Desemba 21 mwaka 2025 hadi Januari 18 ya mwaka 2026 nchini Morocco.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement